Breaking News

MBUNGE JIMBO LA HANAN'G AREJESHA FOMU YA USPIKA MBUNGE

MBUNGE Jimbo la Hanan'g Mkoani Manyara, Mhandisi Samwel Hhayuma, amerejesha Fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Januari 15, 2022, katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Hhayuma amesema  kujitokeza kwa watu wengi katika hatua ya kuomba ridhaa ya chama kuchaguliwa kuwa Spika ni hatua nzuri kwani kuwa na chaguzi nyingi inakuwa inatoa nafasi kupata mtu sahihi.

“Mimi ni mbunge wa Jimbo la Hanang, wana hanang wameniamini, nikipata nafasi ya kuongoza Mhimili wa Bunge maana yake nitawaongoza wabunge wenzangu, ninavyo vigizo vyote vya kuwaongoza, nimekuwa kiongozi toka nikiwa mdogo, hekima na busara za kuongoza ninazo, Mimi najiona Kiongozi.” Amesema Mhandisi Hhayuma
 

No comments