WHO: Dozi Billion 6 Za Chanjo Ya UVICO 19 Zimetolewa Duniani
Shirika la afya Duniani (WHO) limesema mpaka sasa jumla ya dozi za chanjo ya Ugonjwa wa uvico 19 Bilioni 6.3 huku imetolewa Duniani ili kusaidia kupambana na maambukidhi na ugonjwa huo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwakilishi mkazi wa Shirika la afya (WHO) nchini, Dkt. Tigest Mengestu amesema baada ya watu wengi kujitokeza kuchanjwa maambukidhi na idadi ya ya wagonjwa imepungua kwa kasi kutokana na taarifa na tafiti walizozifanya
"Raisi wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amekua mstari wa mbele kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchanjwa na tunajionea wenyewe akiweka mikakati mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma ya kuchanja karibu na wananchi huku vituo vikiongezwa siku baada ya siku" Alisema Dkt. Tigest
Awali akielezea hali ya maambukizi ya Uvico 19 mara baada ya kuanza kuchanja nchini, Mratibu chanjo UVICO 19 Dkt. William Mwegele amesema Mzunguko wa Mdudu katika jamii mara baada ya kuanza kutolewa kwa chanjo unaoyesha kuwa maambukizi yamepungua hivyo wananchi hawana budi kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ili kusaidi kurudi katika hali ya maisha tuliyokua tukiishi awali kutembea bila kuvaa barako
"Mpaka sasa tulipo hakuna dawa tuliyogundua inaweza kutibu ugonjwa wa uvico 19 isipokuwa chanjo hutolewa ili kupunguza maambukidhi na makali ya Ugonjwa ambapo tumeona matokeo chanya sasa baada ya chanjo kutumika". Alisema Dkt. Mwegele
Kwa upande wake Mratibu Matibabu Shirika la afya Duniani Dkt Iriya Nemes amesema zaidi ya asilimia 80 ya watu wanapata ugonjwa huo lakini wanaweza wasionyeshe dalili ya aina yeyote na wana uwezo wa kuwaambukiza wasio na ugonjwa hivyo ni vyema watu kuchukua tahadhari zote za kujikinga dhidi ya maambukidhi hata kama wameshapata chanjo
Pia Dkt Iriya amesema vijana walio wengi wamekua wamekua wakipuuzia chanjo na kujikinga hivyo kupelekea maambukidhi kuendelea katika jamii yao na inayo wazunguka hivyo ni budi waelimishwe zaidi na zaidi
Aidha Shirika la afya WHO limeendelea kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada na mikakati mbalimbali inayojiwekea Kuhakikisha kila mwananchi aanapata chanjo Kwa kuongezea vituo na kuwasogezea huduma walipo na kutoa elimu Maeneo mbalimbali.
No comments