TMA YATOA UTABIRI WA MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA NOV 2021 - APRIL 2022
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakuwa na upungufu wa mvua nchini katika maeneo yanayopata msimu mmoja hali itakayoathiri sekta za uchumi.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akitoa tathimini ya mwelekeo wa msimu wa mvua za mwezi Novemba 2021 hadi April 2022, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema upungufu huo unataraji jitokeza kuanzia mwezi ujao hadi Aprili mwakani.
Ameitaja mikoa itakayoathirika kuwa ni Kigoma, Tabora, Dodoma, Singida, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya pamoja na Iringa ambayo inatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya mikoa hiyo.
Ameitaja mikoa mingine ambayo pia inataraji kuwa na Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa kunyesha pia katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na kusini mwa Morogoro.
"Kunatarajiwa kuwepo kwa vipindi virefu vya ukavu kuanzia mwezi Novemba 2021 hadi Januari 2022, ila kunatarajiwa kutakuwepo kwa ongezeko kidogo la mvua Machi 2022" Alisema Dk. Kijazi.
Aidha Dk. Kijazi aliongeza kuwa mvua zinatarajiwa kuanza kunyesha katika wiki ya tatu ya Novemba katika maeneo mengi na kwisha kati ya wiki ya pili au ya tatu ya Aprili 2022.
Alisema Kutokana na upungufu huo wa mvua TMA imeainisha athari zinazoweza kujitokeza ambazo zinaweza kuathiri ukuaji wa mazao utakaosababishwa na upungufu wa unyevunyevu katika udongo.
"Kufatia kupungua kwa kina cha maji katika mito, mabwawa, hifadhi za maji ardhini hivyo kufanya kuwepo na uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kufatia upungufu wa maji safi na salama,"Alisema Dk. Kijazi.
No comments