Breaking News

NECTA: WALIMU JIEPUSHENI KUTOJIHUSISHA NA UDANGANYAJI WA MITIHANI

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limewaasa walimu wakuu, waratibu elimu na wamiliki wa shule kutojihusisha kupanga na kutekeleza njama za udanganyifu kwenye mitihani ya darasa la nne, kidato cha pili na kidado cha nne inayotarajiwa kufanyika siku za karibuni. 

Akizungumza na waandishi wa wakati akitoa taarifa kuhusu upimaji wa mitihani ya kitaifa itakayoanza Oktoba 28 mpka Desemba 02, katibu Mtendaji wa Necta, Dkt Charles Msonde amezitaka kamati za mitihani za mikoa, halmashauri, manispaa na majiji kuzingatia taratibu zote za uendeshaji wa mitihani ya kitaifa. 

Akizungumzia juu ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani kwa kidato cha nne,pili na Darasa la nne amesema kuwa Jumla ya wanafunzi 1,678,209 wamesajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa darasa la Nne 2021 kati yao Wavulana wakiwa 823085 sawa na aslimia 49.05 na wasichana wakiwa ni 855,124 sawa na asilimia 50.95.

Akizungumzia wanafunzi wa Kidato cha pili amesema Jumla ya Watahiniwa 651,609 wamesajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa 2021,kati yao wavulana wakiwa ni 303,913 sawa na asilimia 46.64 na wasichana ni 347,696 sawa na asilimia 53.36.

Kwa upande wa watahiniwa wa kidato cha Nne Dkt Msonde amesema Jumla ya Watahiniwa 539,243 wamesajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2021 ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 502,316 na watahiniwa wa kujitegemea ni 36,927 .

Hata hivyo Necta imesema Maandalizi yote kwa ajili ya mitihani hiyo ya kitaifa imekamilisha ikiwemo kuandaa na kusambazwa kwa ajili ya mitihani,vijatabu  vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu Upimaji na mitihani hiyo katika mikoa yote Tanzania hata na Visiwani.
 

No comments