Breaking News

MAMA SAMIA ALITAKIA MAFANIKIO TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO, MASTAA KWENDA ROYAL TOUR SAADAN

Rais Samia Suluhu Hassan amelitakia kheri Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Bagamoyo linaloanza kesho.

“Nimeambiwa kuwa kesho mnazindua Tamasha la Utamaduni na Sanaa kule Bagamoyo…nawapongeza. Wizara sasa mmeanza kuwa wabunifu. Endeleeni kufanza vizuri zaidi alisema Mama Samia katika hotuba yake alipokuwa akila chakula cha mchana na Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars.
Rais Samia pia hivi karibuni alishiriki filamu ya kitalii, Royal Tour moja ya vivutio vya Tamasha hilo ni siku ya tarehe 30 ambapo wasanii na viongozi mbalimbali watamuunga mkono kwa kufanya “Bagamoyo Royal Tour” ya kutembelea Hifadhi ya Saadani.

Tamasha hilo limeandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Chuo cha Sanaa (Tasuba).


 

No comments