Wakristo na Waislam Watakiwa Kupendana na Kushirikiana Kulijenga Taifa Kiimani
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Huduma ya Biblia ni Jibu Tanzania Mwinjilisti Cecil Simbaulanga amewakumbusha waamini wa dini kikristo na Waislam nchini kuepuka kujiingiza kwenye migogoro ya kidini na badala yake wapendane na kushirikiana katika kulijenga taifa kiimani.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Mtandao huu jijini Dar es salaam kuhusu mbalimbali ikiwemo Vitabu ambavyo amefanikiwa kuandika kuhusu mambo ambayo wakristo na waislamu wamekua yakiwachanganya hivyo kushindwa kusimamia imani zao.
Alisema tayali nimeandika kitabu kiitwacho "Chanzo cha Mihadhara ya Kidini Tanzania" kwa lengo la kujibu na kuwaelimisha wakristo ambao wamekuwa wakiulizwa maswali kwenye mihadhara na kushindwa kujibu kutokana na kutokua na uelewa mpana juu ya maandiko ya dini.
"Mwaka 1986 Tanzania iligubikwa na mihadhara yakidini iliyoendeshwa na waislam wakitumia Quran takatifu na Biblia takatifu ambapo mlengo wa mihadhara hiyo ilikua ni kuwahoji wakristo juu ya imani yao, mihadhara hiyo ilishamiri hadi mwaka 1992 ndipo nilipoguswa na kuanzisha kikundi cha kujibu mihadhara hiyo" Alisema Mwinjilisti Simbaulanga
Kikundi hicho nilikiita "Biblia ni Jibu" ambapo toka kipindi hicho hadi mwaka 2021 hali ipo shwari kuna mahusiano mazuri kati ya wakristo na waislam, wakristo wanauwezo wa kujibu masuali kutoka kwa waislam, ndipo nilipoamua kuandika kitabu hiki ili wajue namna mihadhara ya kidini ilivyoanza" aliongeza Mwinjilisti Simbaulanga.
Pia ameendelea kusema kuwa amefanikiwa kuandika kitabu kingine alichokiita "Nani mmiliki halali wa mji wa Yerusalem na Nchi ya Israeli"? Waisrael au Wapelestina? Je Biblia takatifu na Quran tukufu vinasemaje? hii ni baada ya kushuhudia makongamano mbalimbali ambayo yalifanywa na waislam hapa nchini mwaka 2004.
Amesema kwamba vitabu vyote vya Quran takatifu na Biblia vinaelezea uhalisia wa umiliki halali wa Mji wa Yerusalem nakwamba Nchi hiyo ni Israel kwahiyo waumini wa dini ya kiislam na wakristo wanaweza kupata nakala ya kitabu hiki ili waweze kujisomea nakujua mambo mengi.
"Naomba kuwasihi waamini wa kiislam na wakristo wenzangu kuacha kuingiza migogoro ya kugombana juu ya mashariki ya kati mwamuzi wa kweli ni kufuata kwenye vitabu vitabu takatifu yaani Quran takatifu na Biblia takatifu" amesema.
"Natoa wito kwa Wakristo na Waislam na hata wasio na dini lakini wanapenda kujua na kusoma maandiko wapate nakala za vitabu hivi wajisomee vitawasaidia kuondoa sintofahamu iliyopo"
Aidha Mwinjilisti Simbaulanga aliongeza kuwa katika kuhakikisha jamii inapata uelewa ameomba kila mwenye mapenzi mema kujitokeza kusaidia changamoto ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuchapisha vitabu hivi vipatikane kwa wingi, atakaeguswa awasiliane nami kupitia namba yangu ya Whatsap 0789606070.
No comments