Breaking News

Serikali ya Awamu ya Sita Kufanya Mapinduzi Makubwa Katika Uwekezaji

Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji mhe. Geoffrey Mwambe ameleza kuwa serikali ya awamu ya sita imejipambanua kuhaakikisha inaweka mazingira wezeshi ya uwekezaji wa maeneo maalum ya viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu juhudi zinazofanywa na ofisi ya waziri mkuu-Uwekezaji pamoja na taasisi zake katika kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji.

Alisema ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na Taasisi zake imeendelea kuboresha na kuboresha uwekezaji nchini kwa kipindi cha mwezi April hadi September 2021 kupitia taasisi zilizo chini yake ambazo ni kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).

Mhe Mwambe aliongeza kuwa ofisi hiyo imeendelea kutekeleza malengo makuu ya uwekezaji ambayo ni matumizi ya uwezo wa nchi yetu katika kuwezesha uwekezaji , kuhamasisha uzalishaji unaolenga kuchochea mauzo ya nje ya nchi, uhamasishaji na uwekezaji kutoka nje ya nchi, uhamasishaji uwekezaji kutika nje, kuhamasisha na kuwezesha maendeleo ya Teknolojia mpya kupitia uwekezaji, Kuinarisha uwazi katika mfumo wakisheria na ulinzi wa mitaji ya uwekezaji na kuimalisha mfumo wa kufatilia vibali vya uwekezaji.

Aidha Mhe Mwambe aliongeza kuwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara kama kufungua akaunti za wafanyabiashara nchini zilizokuwa zimefungwa, hatua ambayo inawezesha kuchochea uchumi na kurudisha imani kwa wafanyabiashara na wawekezaji kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi.

Mhewbe ametoa wito kwa watumishi wa wizara za kisekta kutekeleza majukumu yao kwanufanisi na uzalendo ili suala la wawekezaji ambao ninmtambuka , hivyo kuendelea kuimarisha liwezekuchochea maemdleao ya uchumi.

No comments