Breaking News

OFISI ya Mufti wa Tanzania imefanya dua maalum ya kuwaombea wanafunzi wanaelekea kufanya mtihani wa Taifa wa kumaliza darasa la Saba, kuweza kukabiliana na Mitihani ya kumaliza elimu hiyo ambayo ina anza tarehe 8 Septemba kote nchini.

Dua hiyo iliyofanyika katika msikiti Buza Dar es Salaam iliongozwa na Shekh Shaban Mtambo ikiwa na lengo la kumwomba Mungu awape wepesi katika mitihani yao ambapo shule mbalimbali zilishiriki ikiwemo Amani, kitunda na nyinginezo.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam Mgeni Rasmi katika dua  hiyo, Afisa Uhusiano kutoka OFisi ya Mufti  Shekh Tawfiq Ibrahim amewapongeza vijana hao kufikia hatua hiyo na kuwaombea dua kwa Mungu ya kuongezea Maarifa .

"Kwa kufikia hatua hii leo,tunawaombea kwa Mungu awape wepesi Maarifa, kumbukumbu katika kipindi chote cha mitihani yenu" Alisema Tawfiq.

Aidha, Tawfiq amewataka vijana hao kumtanguliza Mungu na kufanya jitihada za kujisomea ili kukabiliana na mitihani hiyo na kuongeza kuwa matokeo Bora uandaliwa kwa kujisomea kwa bidii.
Kwa upande wake Mratibu wamfuko wa kusaidia wanafunzi wa Dini ya kiisilamu (TESA), Ramadhani Abdallah amewataka vijana hao kuoondoa hofu wanapo kuwa katika vyumba vya Mitihani.

Alisema wanafunzi watakafanya vizuri taasisi hiyo hutoa ufadhili kwa wanafunzi kwa wale watakao chaguliwa kuendelea na Masomo ya Sekondari alisema hivi sasa kunawanafunzi wanaodhaniwa na taasisi ilikufia Malengo Yao.
Naye Muandaaji na muhamasishaji kutoka taasisi ya TAMSYA, Sheikh Mikidard Khaflan amewataka nakutakia heri na mafanikiovijana hao kipindi chote ambapo nikawaida kuandaa dua kuwa kawaida yake kuandaa dua ya kuwa ombea Dua wanafunzi wa nao hitimu Masomo yao.

Mmoja wanaotarajiwa Kufanya Mitihani hiyo Ramadhani Abdallah kutoka shule ya Msingi Amani Dua hiyo itawafungulia Milango ya kheri katika kukabiliana naMitihani hiyo ameitaka jamii kuiga mfano huo ambao kuwaweka vijana katika utayari  Kufanya vizuri.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba kutoka shule mbalimbali walioshiriki katika dua hiyo.

No comments