Breaking News

Serikali Kuunda Mfumo Utakao Kuendeleza Falsafa Ya KAIZEN Nchini

Serikali imesema kuwa kupitia Wizara za Viwanda na Biashara, Fedha na Mipango na Afya, pamoja na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hizo wameamua kuunda mifumo ya kuendeleza falsafa ya KAIZEN nchini ili kuhakikisha kuwa falsafa hiyo inaoanishwa kwenye Sera mbalimbali za nchi sambamba ili iweze kusaidia jitihada za Serikali za maendeleo.

Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (UWEKEZAJI) Willium Tate Ole Nasha amesema hayo wakati akifungua Kongamano la KAIZEN Barani Afrika kwa mwaka 2021 (AKAC2021) lililofanyiaka kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam na kuyakutanisha Mataifa zaidi ya 20 yanayotekeleza falsafa hiyo.

Alisema Serikali inatambua ni jukumu lake la kuboresha mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya nchi na uwekezaji ili kuifanya nchi kuwa ya ushindani zaidi katika uzalishaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.

 Serikali itaendelea kutoa miongozo na sera mbalimbali na kusimamia utekelezaji wake kwa kila sekta ikiwemo kutoa dira ya namna ambayo kila mhusika atakavyowajibika katika kukabiliana na mapungufu yaliyoko katika eneo lake ili kutatua kero za wananchi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi inaendeleza sekta ya viwanda kulingana na hali halisi ya soko la Dunia na malengo ya mipango mipana ya maendeleo ya nchi yetu” Alisema Ole Nasha.

Alisema kuanzia mwaka 2007 katika sekta tofauti tumeanza kuitekeleza hii falsafa na tumeboesha huduma, tumeongeza mapato na kuokoa muda kwa hiyo msingi wa  falsafa ya KAIZEN ni kuona namna gani unavyoweza kujipanga katika mambo haya na hiyo ndio KAIZEN.

Mhe. Ole Nasha aliongeza kuwa Serikali inakumbatia farsafa ya KAIZEN kwa sababu inaenda sambamba na mtizamo wao wa namna ya kujenga Taifa la Viwanda, lenye uchumi unaoweza kushindana, Taifa lenye uwajibikaji na Taifa linaloweza kushindana kiuchumi na nchi nyingine hivyo kuwa na imani kila mtu akipata farsafa ya KAIZEN atatimiza wajibu wake wa kuhakikisha anajipanga kutekeleza majukumu yake.

“Sisi kama Serikali tunajipanga tunahimiza hayo yote kwa watanzania tunataka wizara na idara zetu zihakikishe kwamba zinafuata farsafa ya KAIZEN kwa sababu tunahitaji tija tunahitaji kukata gharama tunahitaji uwajibikaji tunahitaji kuwajibika ndio maana leo hii tumefarijika kuandaa mkutano kama huu na Mhe. Rais Samia anafahamu farsafa hii” ameongeza Mhe. Ole Nasha.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke alisema falsafa za kijapani zimekuwa zikisaidia sana kuratibu masuala mbalimbali lakini pia kuongeza ufanisi na kwamba makongamano kama hayo yanawapa fursa na viongozi kuweza kujifunza namna ambavyo falsafa hizo kuweza kuwasaidia wananchi.

“Sisi kwenye halmashauri zetu shughuli kubwa ya wananchi wetu ni biashara sasa tunatoa hela nyingi kwa makundi ya kinamama vijana, na makundi mamalumu, sasa tuangalie jinsi gani farsafa hizi zinaweza kuwasaidia wananchi wetu kuweza kufikia malendo yao ya kibiashara” Alosema DC Jokate.

Alisema natamani sana mfike kwenye manispaa zetu ili tushirikiane kuwajengea uwezo wa namna gani ya kufikia malengo yao hasa kupitia farsafa hizi na hasa makundi haya ambayo yamekuwa yakijishughulisha na biashara zao kwa kuwezeshwa na manispa zetu kupitia ile mikopo ya halmashauri.

No comments