Rc MAKALLA Azindua Mfumo Wa Ukusanyaji Ushuru Wa Maegesho Kidijitali
-Alisema Mfumo huo pia utasaidia kuwadhibiti Vishoka.
-Ushuru wa Maegesho Sasa kupokelewa moja kwa moja serikalini.
- Alisema Mfumo utaondoa Rushwa, uonevu na utaongeza ufanisi na ongezeko la Mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo August 24 amezindua mfumo rasmi wa ukusanyaji wa malipo ya Ushuru wa Maegesho kupitia njia ya Simu ambapo amesema Mfumo huo utakuwa suluhu ya tatizo la Vishoka waliokuwa wakijipatia pesa ya Maegesho kwa njia ya udanganyifu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, RC Makalla amesema Mfumo huo utaanza rasmi kutumika Jijini humo September mosi mwaka huu na utaenda kutatua kero na changamoto mbalimbali.
Miongoni mwa Changamoto ambazo RC Makalla amesema zitakwenda kumalizwa na Mfumo huo ni Rushwa na mianya ya Upotevu wa Mapato uliokuwa ukisababishwa na Ukusanyaji kwa njia ya Cash ambapo mtu alikuwa na uwezo kufikisha Serikali kiasi kidogo Cha fedha kuliko kile alichokusanya.
Aidha RC Makalla amesema Mfumo huo utatoa pia ufumbuzi wa kero ya uonevu na manyanyaso yaliyokuwa yakiwakuta Wenye magari Kutokana na uwepo wa Watumishi wasiokuwa waadilifu.
Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kuwasisitiza TARURA na Halmashauri za Dar es salaam kukamilisha utaratibu wa kuweka Vibao vya Wrong Parking kwenye maeneo yote yasiyoruhusiwa kuegesha magari.
Mfumo wa Malipo ya Ushuru wa Maegesho kidigital unasimamiwa na TARURA na unamuwezesha Mwananchi kulipa kwa njia ya Simu ya mkononi au njia ya Bank ambapo baada ya kufanya malipo utapokea ujumbe ukikuonyesha kuwa malipo yamefika serikalini
No comments