Dc Fatuma Nyangasa Awataka Wanawake Kiislamu Kufuata Mafundisho Ya Dini.. Kupata Mwongozo Sahihi Katika Kuzilea Familia Zao
MKUU wa Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam Fatuma Almas Nyangasa amewataka akina mama wa dini ya kiislamu kuwa na misingi ya imani katika kukisoma na kukijua kitabu cha mungu ili waweze kupata muongozo sahihi wa maisha katika kuzilea familia zao.
Hayo yamebainishwa Mkoani Dar es Salaam katika mashindano ya 9 ya usomaji wa Kur-an yaliyokuwa yameandaliwa na taasisi ya Tanzania Holy Qur'an Competition for women yaliyofanyika katika ukumbi wa City Garden amesema wanawake wananafasi kubwa katika malezi ya familia na jamii.
Mshindi wa kwanza wa juzuu 18 katika mashindano hayo ni Kioni Sharif kutoka Zanzibar ambaye alijipatia kiasi cha shilingi laki 5 pamoja na kiwanja na wapili juzuu 18 Mariam Ibrahim wa Dar es Salaam alijishindia shilingi laki 4 pamoja na mashine ya kudarizi huku mshindi wa tatu wa juzuu 18 Sada Hamad wa Dar es Salaam alijipatia Shilingi laki 3 na mashine ya kudarizi.
"Mashindano ya tisa kwa wanawake yanaleta matumaini mema na mazingira mazuri ya kumjua mungu sambamba na kujua thamani ya viumbe na kuumbwa kwao, naishukuru taasisi hii kwa kutekeleza azma ya mashindano haya kwa kundi la akinamama," amesema Nyangasa
Aidha Nyangasa amesema kwamba ni vema kuendelea na programu hiyo kwa vizazi vyetu na kuwataka akinamama kuwa mabalozi wazuri kwa wengine katika kuendeleza na kuhamasisha usomaji wa kitabu kitukufu cha mungu kinachofundisha mantiki ya kujua thamani ya kuumbwa kwao na kumtumikia mungu kipindi chote cha uhai.
Kwa upande Mratibu wa mashindano hayo Mohammed Ally amesema kuwa lengo kuwa la mashindano ni kuwahamasisha akinamama kukisoma kitabu kitukufu cha mungu na kutambua ndio silaha pekee ya kuhitaji msaada wake.
Aliongeza kwamba mashindano ni mwaka wa 9 toka yamenza hivyo amesisitiza makundi ya akinamama kupenda kusoma kitabu cha Qur-an ili waweze kupata radhi zake.
Nae mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Kioni Sharif kutoka Zanzibar amesema kwamba amejisikia faraja kubwa na kuwahamasisha wanawake kusoma kitabu cha mungu kwa ajili ya kupata faida katika ulimwengu huu.
No comments