Serikali Yakusanya Bil 48 Kutokana Tozo
Dar es salaam: Na Timothy Marko
Serikali imesema tayari imekusanya shilingi Bilioni 48.489 kutokana nakuwepo kwa tozo za mihamala ya simu kwa kipindi cha July Hadi Agost Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba alisema kutokana na makusanyo hayo tozo za mihamala Fedha hizo zinatarajiwa kuwekezwa katika ukarabati wa vituo vya Afya zaidi ya 90 huku shilingi Bilioni Saba zinatarajiwa kuwekezwa kwenye ujenzi wa Madarasa Maeneo ya vijijini.
"Kutokana na Sheria hii ya mihamala ambapo Sheria hii imekuwa ikitumika Tanzania bara na Zanzibar ambapo Fedha hizo Zanzibar imekusanya bil 1.6 katika kipindi cha miezi minne". Alisema Waziri Nchemba
Nchemba alisema katika Fedha hizo, Zanzibar imekusanya inatarajia kujenga Vituo vya afya 150 pamoja na Madarasa 500.
Alisema katika kipindi cha mwezi moja mihamala milioni9.9 imeongezeka Hadi milion 10.5 nakuweza kuzalisha milioni48 .
"Tunaendelea kulipa madeni ya bil 600 ya Makandarasi". Aliongeza Waziri Nchemba.
No comments