RC MAKALLA: Wezi Wa Mafuta Bandalini Kukiona
Kamati ya uchunguzi imekamilisha kazi na Ripoti kukabidhiwa mamalaka za Juu.
Aipongeza Mamlaka ya Bandari kutekeleza maagizo ya Kuu Mkoa kununua kifaa cha kubaini wote walio na watakaochepusha Mafuta kutoka Bomba kuu.
Awataka wote Waliojiunganishia mabomba Katika Bomba kuu kujisalimisha.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo August 20 ameshuhudia na kukagua kifaa Cha Kisasa Cha kubaini wizi na upotevu wa Mafuta ghafi (Radio detector) kutoka bomba kuu la kupokea Mafuta kutoka kwenye meli kuelekea kwa Wafanyabiashara ambapo kifaa hicho kinatarajiwa kuanza zoezi la ukaguzi muda wowote kuanzia leo.
Upatikanaji wa kifaa hicho ni Kufuatia maelekezo aliyotoa RC Makalla kwa TPA baada ya kuunda kamati ya ufuatiliaji upotevu wa Mafuta ambapo miongoni mwa mapendekezo ya Kamati ilikuwa ni ununuzi wa kifaa cha kudhibiti wizi wa mafuta bandarini.
Aidha RC Makalla amewahakikishia Wafanyabiashara wa Mafuta kuwa Serikali imejidhatiti kumaliza kabisa tatizo la upotevu wa Mafuta na anashukuru kuona adi Sasa kumekuwa na matokeo mazuri
Hata hivyo RC Makalla amesema hadi Sasa tayari Vyombo vya ulinzi na usalama vimewakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa Wizi huo.
Katika ziara aliyofanya RC Makalla bandarini siku ya leo ametembelea pia Ujenzi wa Barabara za kuingia na kutoka bandarini na upanuzi wa eneo la kushusha na kupakia Mizigo ambapo ameipongeza Mamlaka ya Bandari kwa Mapinduzi makubwa ya maboresho ya huduma kwa Wananchi.
No comments