Chama cha AFP Chatoa Ushauri Kwa Serikali Kuhusu Chanjo ya Uviko 19
Chama cha Wakulima Tanzania (AFP) kimeishauri serikali kuacha kupambana na baadhi ya watu ambao wanapotosha jamii juu ya chanjo ya Uviko 19 na badala yake iendelee kutumia wataalamu wake wa afya kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo hiyo.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mhe.Rashid Ligania katika mahojiano na mwandishi wa mtandao huu kufuatia hali ambayo upotoshaji sintofahamu kufatia kuwepo na upotoshaji hususani katika mitandaojuu ya chanjo ya Uviko 19 kuwa na madhala makubwa ikiwemo kuganda kwa damu pindi mtu atakapochanjwa.
Alisema watu hao wakiwemo wanasiasa wamekua wakitumia kipindi hiki kutoposha juu ya chanjo hiyo kwa maslahi yao binafsi hivyo serikali isiendelee kupoteza muda kukabiliana nao bali iendelee kutoa elimu juu ya chanjo hiyo kwani kuchanja ni hiari na sio lazima.
"Wanasiasa wengi wanatumia agenda hii kupotosha umma na kuharibu jitihada za serikali za kuokoa afya ya wananchi wake, pia wanataka kuzungumziwa wao kwenye mitandao ya kijamii ili kupata kiki kuelekea uchaguzi mkuu 2025 , hivyo hawa sio wazuri wanatakiwa kupuuzwa na serikali na kuendelea kutoa elimu juu ya chanjo hii"alisema.
Kuhusu hali ya siasa nchini katibu mkuu huyo alisema hawezi kuzungumzia mikakati yoyote kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kutokana na kwamba hali ya siasa bado ni mbaya kwa sababu vyama vya siasa hasa vya upinzani kumekuwepo na zuio la kufanya mikutano kwa muda mrefu sasa.
Alisema vyama vimekosa nguvu kutokana na zuio hilo hivyo kungoja hadi vipate maelekezo kutoka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) pindi inapotokea uchaguzi wa muda kama kuna mbunge au diwani kafukuzwa chama au kafariki dunia.
"Kwasasa tuna subiri hadi itokee labda kuna uchaguzi mdogo ndo tunaruhusiwa kujitokeza kufanya kampeni, vyama vyetu havina uwezo wa kifedha hivyo kushindwa kushiriki kikamilifu katika chaguzi jambo linalopelekea kushindwa kushika dola, tunaomba turuhusiwe kufanya mikutano yetu ya ndani na nje" alisema.
No comments