TBS Yawataka Watumiaji wa Vipimo Sekta ya Afya kuhakikisha Ubora Wa Vipimo

Kuelekea Siku ya Vipimo Duniani Mei 20, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka watumiaji wa Vipimo katika sekta ya afya nchini kuhakikisha vipimo hivyo vimepitishwa na Shirika hilo kabla havijatumika.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mkumba amesema wamekuwa wakikutana na Changamoto kubwa ya watumiaji wa Vipimo kutokuwa na uwelewa wa kufanya uhakiki wa vifaa vyao ili kuboresha huduma wanazozitoa kwenye sekta za afya.

“Vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya ni muhimu vikahakikiwa na kujulikana ubora wao kwa kufanya hivi itakuwa inalinda afya ya wagonjwa kwasababu daktari anaweza kufanya maamuzi kupitia vipimo vinavyotoka maabara vikiwa vipimo sio sahihi vinaweza kupelekea kumpatia madhara mgonjwa”. Amesema Bw.Mfaume

No comments