Wadau wa Utalii waishauri serikali ya rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama  Samia Suluhu Hassan ameombwa kuhamasisha wafanyakazi ambao wanapata fursa za semina mbalimbali  waweze kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo kwenye hifadhi za Taifa  mara baada ya kumaliza mafunzo yao.

Hatua hiyo itasaidia kuongeza mwamko wa utamaduni kwa watanzania kupenda kupanga  kutembelea hifadhi za Taifa kama wanavyofanya raia wa kigeni wanaokuja kutalii nchini nakuweza kukuza sekta ya utalii.

Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es slaam na Bi. Isabela Mwampamba ambaye ni mtanzania wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya covid 19 alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitokea nchini Ubelgiji nakusema kwamba sekta ya utalii  bado imeathirika kwa kiwango kikubwa baada yakuingia virusi hivyo.

Aliendelea kuieleza Tanzanite  kwamba wafanyakazi ambao wanapata fursa za semina  kutoka katika mikoa mbalimbali wajengewe utamaduni wa kutembelea hifafhi za taifa zilizopo katika mikoa ambamo semina hizo zinafanyika mara baada ya kumaliza  semina.

Bi Isabela Mwampamba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule ya Upendo Friends International iliyopo mkoani Arusha  alisema kwamba jamii iwe na mwamko wa kupanga kutembelea vivutio vya utalii nakuachana na mambo ya kwenda kwenye maeneo ya  anasa akitolea mfano baa.

Alisema kwamba wafanyakazi ambao wanahofia gharama za utalii  wanaweza kujiunga kwenye makundi kwani kufanya hivyo inasaidia  wao kuweza kumudu gharama hizo bila shida yoyote.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Utalii wa Puto ( Balloon Safari Advanture Aloft) Samson Mollel alisema kwamba utalii wa puto (balloon safaries) ni mzuri zaidi sana lakini  unakua na gharama kubwa tofauti na utalii wa kutembea kwanye njia za hifadhi.

"Utalii wa puto niwakusafiri juu ya hifadhi kwa kutumia puto( balloon), utalii wa aina hii una gharama tofauti na ule wa kawaida manake gharama yake ni dola 550 sawa na  shilingi milioni moja na laki mbili hivi au zaidi kwa raia wa kigeni halafu kwa watanzania ni shilingi laki tisa." Alisema Bw.Mollel

Nakuongeza kwamba " Watanzania wengi wanashindwa kutembelea hifadhi za Taifa kwasababu ya hali zao duni za  uchumi tunaomba TANAPA na mamlaka zingine wajaribu kushusha bei ili kuweza kusaidia kuongezeka kwa watanzania ambao wanapenda kutalii.

No comments