Breaking News

Wafanyabiashara Wapunguziwa Tozo Maonyesho ya Sabasaba Mwaka Huu


Na: Hussein Ndubikile
Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) imepunguza tozo ya wafanyabiasha kwenye mabanda ya maonyesho sabasaba ili kusaidia kuongeza ushiriki wa Makampuni ya wawekezaji na wajasriami wadogo Nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Naibu waziri wa Viwanda na biashara Stella Manyanya lisema  maonyesho hayo ya 44  yalitakiwa yasifanyike kutokana na changamoto ya ugonjwa wa covid 19 kutokana na eneo hilo lilitengwa kwa tahadhari ya kuwahifadhi wagonjwa .

Alisema lakini jambo la kumshukuru Mungu ugonjwa umepungua na maonyesho yataendelea kuanzia julai 1-7 mwaka huu na asilimia 75  ya makampuni ya ndani yameshaonyesha nia kushiriki.

"Katika kipindi hicho baadhi ya wafanyabiashara waliyumba na makampuni mengi yalipunguza wafanyakazi hivyo mamlaka kwa kutambua changamoto hiyo imepunguza tozo katika ushiriki wa maonyesho kwa mwaka huu," alisema Eng. Manyanya.

Alisema   wafanyabiashara wasiogope wajitokeze kutangaza bidhaa zao kwani itawapa wigo mpana wa kongeza soko na kukuza mitaji yao.

Hata hivyo alisema maonyesho ya biashara mwaka huu yamekuja tofauti sana kwani kutakuwa na kuonyesha bidhaa kwa njia ya mtandao ili wateja popote walipo hata nje ya nchi waone bidhaaa za wakulima kwa njia ya mtandao ikiwemo mpunga.

Kwa upande wake naibu Mkurugenzi wa (TANRTADE) Latifa Hamisi  ametoa wito kwa wafanyabiashara na wakulima kushiriki kwa wingi katika maonyesho hayo kwani gharama ni nafuu kwa mwaka huu kwa malekezo zaidi na tatizo wafike mamlaka hiyo.

No comments