Breaking News

Prof.Lipumba: Bado Tuna Tatizo la utekekezaji Mipango wa maendeleo kuathiri Kufikia Malengo


Profesa wa Uchumi na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema tatizo la utekelezaji wa mpango wa kwanza wa Maendeleo wa Serikali utasababisha malengo muhimu ya mpango wa pili wa Maendeleo ya Serikali kutofikiwa.


Akizungumza makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es Salaam wakati akichambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2020/21 ambapo amesema tatizo la utejelezaji limeendelea kuathiri mpango wa pili wa miaka mitano kutokana na mpango huo kuteua baadhi ya miradi kielelezo ambayo awamu ya kwanza haikutekelezeka na kuhamishiwa awamu ya pili.

Aidha ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma liganga, maeneo ya uwekezaji bandari Bagamoyo, Mtwara, Kigoma na Mwanza, Kituo cha biashara na huduma Kurasini, ujenzi wa Reli ya kati na matawi yake kwa kiwango cha Standard Gauge, Mji wa kilimo Mkulazi, Ufufuaji wa Shirika la Taifa la Ndege na kusomesha vijana wengi katika fani ya ufundi stadi katika maeneo ya kipaumbele.

Prof. Lipumba amesema malengo ya mpango wa pili hayatafikiwa ikiwemo ukuaji wa pato la taifa la asilimia 10 mwaka 2020, ukuaji wa sekta ya viwanda kwa asilimia 10.5 na sekta ya Kilimo kukua kwa wastani wa asilimia 7.6.

Hata hivyo amesema Hotuba ya Rais wakati alipozindua Bunge alieleza mwongozo mzuri wa viwanda vitakavyojengwa ambapo miongoni mwake zitatumia malighafi za ndani takribani miaka mitano sasa uzalishaji wa nguo umeporomoka toka eneo la mraba 119.5 milioni mwaka 2014 hadi eneo la mraba 45.4 milioni mwaka 2019.

Prof Lipumba ameongeza kuwa hotuba ya bajeti ya Serikali haikuongozwa kwa lengo la kutekeleza mpango wa pili wa Maendeleo kutokana na hotuba nyingi za wizara kutojikita katika kueleza utekelezaji wa mpango wa Maendeleo ambapo miradi mitatu tu ndio iliyopewa kipaumbele ununuzi wa Ndege, Ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge na ufuaji wa umeme wa Stieglers Gorge.

Sambamba na hayo amesema bajeti ya Maendeleo inategemea mikopo ya ndani na nje kutokana na mapato ya ndani kukidhi kugharamia matumizi ya kawaida na ulipaji wa madeni na hakuna fedha inayobaki kugharamia mpango wa Maendeleo.

Aidha amesema idara na mashirika ya Serikali hayana uhakika wa bajeti zao kutokana na Wizara nyingi zinapata fedha kidogo kuliko zile zinazoidhinishwa na Bunge pamoja na wingi wa malimbikizo ya madeni ambayo hayajalipwa.

Prof Lipumba ameongeza kuwa mazingira ya kufanyia biashara Tanzania ni magumu kutokana na ripoti ya Benki ya Dunia ya mazingira ya kufanya biashara ya mwaka 2020 Tanzania kuwa nchi ya 144 kati ya nchi 190.

Kwa upande nwingine Prof. Lipumba amesema ushirikiano wa nchi na taasisi washirika wa Maendeleo umedorora kutokana na hadi sasa Tanzania kutopata msaada toka benki ya Dunia na shirika la fedha la kimataifa kukabiliana na janga la corona.

Hata hivyo amesema Chama cha CUF kimeandaa jopo la wataalamu wanaopitia sera ya furaha na haki sawa kwa wote ambayo pamoja na mambo mengine imejikita katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yanaunga mkono itikadi ya utajirisho na sera ya haki sawa na furaha kwa wananchi.

No comments