Breaking News

Mhe Hamad Rashid Aongoza Kikao cha Kamati Tendaji Taifa Ofisi Kuu za chama Zanzibar


Kikao cha Kamati Tendaji Taifa kilichokaa tarehe 06.06.2020 chini ya Mwenyekiti wa chama Taifa Mheshimiwa Hamad Rashid Mohammed na kuhudhuriwa na viongozi wote wa ngazi ya juu ya chama Taifa katika Ofisi Kuu za chama Zanzibar kilifikia maazimio yafuatayo:
1. Kusimamisha Wagombea wa nafasi za Urais Muungano na Zanzibar, Ubunge na Uwakilishi pamoja na Udiwani katika Kata za Bara na Wadi kwa Zanzibar. 
2. Kutengeneza kanuni za Uchaguzi ndani ya chama kwa mwaka 2020
3. Kumalizia ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020.
4. Kutoa utaratibu wa mchakato wa uchaguzi ndani ya chama kupata wagombea watakaowakilisha chama katika nafasi mbalimbali za serikali.
5. Kamati tendaji pia imependekeza kuwa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea hautakoma kuendana na kalenda ya chama hadi pale kalenda ya Tume ya Uchaguzi Taifa itakapokoma.

Kutokana na maazimio hayo leo tarehe 14.06.2020 tumekamilisha maagizo ya Kamati Tendaji Taifa hivyo tunawaarifu wanachama na wananchi wote kwa ujumla wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za serikali wajitokeze kupitia chama cha ADC. 
Aidha katika mashirikiano ya chama chetu na vyama vingine milango iko wazi kwa chama chenye nia ya dhati tofauti na mashirikiano yaliyowahi tokea huko nyuma mfano ukawa kusababisha vyama vingine kuburuzwa.

ADC - Dira ya Mabadiliko 
ADC  - Tumaini la Mtanzania 

Imetolewa na;
Mkurugenzi wa Habari ADC - Makao Makuu
Aisha Mbegu.

No comments