SEKTA YA HABARI KINARA UVUNJAJI SHERIA YA AJIRA
Dar es salaam - Chama cha Wafanyakazi kwenye vyombo vya habari (JOWUTA) kimesema sekta ya habari inakabiliwa na tatizo kubwa la kutotekeleza Sheria ya ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004 Jambo linalochangia maslahi na mazingira duni ya kazi.
Mbali na hayo kutotekelezwa Kwa Sheria hiyo pia kumeifanya sekta ya habari kushindwa kutoa mchango wa kutosha katika uchumi wa taifa.
Katibu Makuu WA JOWUTA Selemani Msuya ameeleza hayo Desemba 18, mwaka huyu, alipokuwa akiwasisilisha salamu za chama hicho katika mkutano wa wadau wa sekta ya Habari na Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Mchezo Profesa Palamagamba Kabudi.
No comments