Nccr Mageuzi Kusimamisha Wagombea Katika Nafasi Zote Uchaguzi Mkuu 2020.
Chama cha NCCR Mageuzi kimesema kitasimamisha wagombea katika nafasi zote Tanzania bara na Zanzibar katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika chini mwezi Octoba.
Akizungumza na waandishi wa habari kibaha mkoani pwani katibu mkuu wa chama hicho Bi. Elizabeth Mhagama alisema chama kimejipanga kuakikisha kinashiriki uchaguzi kwa mujibu wa sheria na kanuni hili kuweza kuwapatia wananchi kuchagua viongozi bora.
"Katika mkutano mkuu wa halmashauri kuu ya chama ulioketi mapema mwezi ilipitisha kwa kauli moja na kiadhhimia kushiriki na kitasimamisha wagombea katika nafasi zote za uchaguzi utakaofanyika mwezi octobar mwaka huu" Alisema bi. Mhagama.
Katibu mkuu wa Chama cha Nccr Mageuzi, Bi. Elizabeth Mhagama akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA bw. Joackim Mahega.
Alisema pamoja na kusimamisha wagombea pia mkutano uliwataka viongozi wote wa chama kuanza mara moja kutafuta wananchama kuanzia kwa wahasisi wa chama tangu mwaka 1995 na wanachama wapya wanaotaka kujiunga na chama hicho.
"Chama cha NCCR baada ya kujitafakali na kuangalia sababu zilizopelekea kufikia tulipo tumejifunza na tunaomba radhi watanzania na kuhaidi kutokurudia makosa tuliofanya mwaka 2015"
Bi Mhagama aliongeza kuwa mara kikao hicho pia kiliagiza viongozi woke kuhakikisha wanaanza kampeni ya kuwarudisha wanachama na viongozi wote walikuwa chama tangu mwaka 1995 pamoja na kutafuta wanachama wapya.
Katika hatua nyingi chama hicho kimepokea wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali pamoja na aliyekuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema bw. Joackim Mahega na kumkabidhi kadi ya chama cha NCCR Mageuzi.
No comments