Breaking News

WEMI TZ Yagawa Barakoa Bure Kwa Yatima, Bodaboda


Taasisi ya Worship Empowerment Ministry Tanzania (WEMI TZ) jana imegawa vifaa vya kuzibia mdomo  'barakoa'  katika vituo vya Watoto Yatima vya Umra, Al-Madina na Sifa Group Foundation vilivyoko Vikawe Bagamoyo mkoani Pwani na baadhi ya vituo vya bodaboda.

 WEMI imegawa barakoa hizo ikiwa ni sehemu ya Juhudi ya kuiunga mkono Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Janga hatari la Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Korona.

Akizungumza kwa niaba ya Mwanzilishi wa WEMI, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili na Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la Revival , Milca Kakete,  Mwakilishi wa WEMI Kijiji Dar Es Salaam, Mlapa Ng'osha.

Alisema WEMI imeguswa na Namna  Serikali ya  Rais, Dk John Pombe Magufuli na Wizara ya Afya jinsi inavyopambana na ugonjwa wa korona ikiwemo kumtanguliza Mungu kama kinga, tiba na mtetezi mkuu,  kutoa Elimu kwa sekta na Makundi Mbalimbali.
"Tumeamua kuiunga mkono serikali  Yetu ya Rais Dk, Pombe Magufuli kupambana na Janga la korona. Kama WEMI tumegawa Barakoa 200 katika ili kuwasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa KUPATA Vifaa hivyo.

"Barakoa hizo tumegawa katika Vituo vya Watoto Yatima vya Umra, Al-Madina na  Sifa Group Foundation vilivyopo, Vikawe, Bagamoyo mkoani Pwani pamoja na Vituo kadhaa vya Dereva pikipiki (bodaboda).

"Serikali imejitahidi kwa sehemu yake lakini na sisi kama WEMI tumeguswa na tumeamua kujitoa kuhakikisha Tanzania na Watanzania wenzetu wanabaki salama.
Tutaendelea kutoa Elimu stahili kwa kufuata muongozo wa Wizara ya Afya, pia tunampongeza Waziri wake Ummy Mwalimu pamoja na timu nzima kwa Namna inavyopigana. Alisema Mlapa.

Taasisi ya WEMI Tanzania  yenye  makao makuu nchini Canada, imekuwa ikiwawezesha Waimbaji wa nyimbo za Injili na Wachungaji wa Vijijini wanaotoa huduma ya Mungu katika mazingira magumu.
WEMI imekwishagawa baskeli kadhaa kwa baadhi ya wachungaji na kumuwezesha kiuimbaji Mwimbaji Mwenye ulemavu wa macho, Paschali wa Dodoma aliyeimba wimbo wa Nakung'ang'ania remix.

Hata hivyo, WEMI wamejipanga pia kutoa barakoa na vitu vingine katika vituo baadhi ya Mkoa wa Dodoma.

No comments