Breaking News

Wanafunzi wa Taaluma ya Shahada ya Bunifu UDSM Watakiwa Kulitumia Tamasha La Sanaa Blast Kama Fursa Ya Kujiajiri

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) wanaochukua Shahada ya Sanaa Bunifu wameaswa kulitumia Tamasha la Sanaa Blast kama fursa ya ajira kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.

Aidha, wametakiwa kuachana kutumia vionjo vya nje ya nchi katika kazi zao za badala watumie vionjo vya asili ili waweze kujitofautisha na kazi za wasanii nje.

Hayo yamesemwa na Principal wa Ndaki ya Hisia- Idara ya Sanaa Bunifu wa chuo hicho, Dkt. Rose Upor katika Siku ya Kwanza ya tamasha hilo.

Amesema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kulitumia tamasha kama fursa ya ajira kwani kupitia Sanaa Blast wanafunzi wanapata fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwenye sanaa ya muziki, uchoraji na uigizaji na kubainisha kabla au baada kuhitimu wana uwezo wa kujiajiri kutokana mafunzo ya vitendo waliyopata.

“ Wanafunzi wanatakiwa kulitumia tamasha hili kujiajiri kwa sababu mafunzo wanayopata kwa vitendo kwenye taaluma yao yatawasaidia kujiajiri na kutengeneza ajira,” amesema Dkt. Rose.

Amebainisha kuwa lengo la tamasha hilo kuviendeleza vipaji vya wanafunzi wa taaluma hiyo, kuwawezesha wanafunzi kufanya sanaa ya vitendo baada ya kuhitimu pamoja kuwajengea uwezo wa kujiajairi baada ya kuhitimu.

Amesisitiza kuwa tamasha hilo ni endelevu na kwamba mwakani litaboreshwa huku na kwamba mwaka watatoa tuzo mbalimbali katika sanaa ya uchoraji, uigizaji na muziki.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Sanaa Bunifu ya chuo hicho, Dkt. Kelnony Mapana amesema idara hiyo inawasisitiza wanafunzi kufanya kazi zao kwa weledi pasipokutumia lugha za matusi na kuiga vionjo vya wasanii wa nje kwani wakifanya hivyo watapoteza uhalisia wa kazi zao.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (Basata) Godfrey Mngereza amepongeza idara hiyo kwa kufanya tamasha hilo kwani linawejengea wanafunzi uwezo na kujiamini katika soko la ajira.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini, Kiago Kilonzo ameipongeza idara hiyo kwa juhudi za dhati za kutengeneza vipaji vya wanafunzi wa taaluma ya sanaa kupitia tamasha hilo.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Adrian Nyanang’ale ameiomba idara hiyo kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu na litalokuwa na tija kwa wanafunzi wa taaluma ya sanaa bunifu.

Naye Mratibu wa tamasha hilo, Catherine Kahabi amewaomba wanahabari kuhudhuria shughuli ya utoaji tuzo hizo na kwamba kufanya hivyo kutasaidia kuitangaza sanaa hiyo.


Pia amesema kuwa wanahabari wanatakiwa kutoa sapoti katika taaluma ya sanaa bunifu ili kuwatengeneza soko la ajira kuek wanafunzi wenye vipaji vya uchoraji, muziki na filamu wakati nchi ikielekea katika uchumi wa viwanda





No comments