Breaking News

Shirikisho La Wenye Viwanda CTI Laipongeza Bajeti Ya Serikali Mwaka 2019/20


Shirikisho la wenye Viwanda nchini (CTI), limeipongeza bajeti ya serikali ya mwaka 2019/2020 kuwa imekidhi matakwa ya shirikisho hilo huku ikiitaka serikali kuhakikisha inavilinda viwanda vya ndani hususani katika viwanda vya chuma ambapo katika nchi za wengine vimekuwa vikisaidiawa na serikali zao.

Akizungumza jijini Dar es salaam mkurugenzi mtentendaji wa CTI, Leodegar Tenga amesema kuwa mbali na kulinda viwanda   serikali  iwasadie kupunguza kodi ya kuingiza mafuta ghafi kutoka nje ya nchi ili kupunguza gharama za uendeshaji na  kuweza kushindana na masoko mengine ya nje ya nchi.

Aidha CTI imeiomba serikali  kupunguza utiti wa vyombo vya udhibiti wa bidhaa jambo ambalo linaongeza ulasimu  huku wakiishukuru serikali kwa  kuondoa tozo 54 ambazo zilikuwa zinawaelemea wenye viwanda Jambo ambalo awali halikuwepo.

Naye kaimu Mwenyekiti wa CTI Shabbir Zavery  amesema bajeti ya sasa imewafurahisha kwa kuwa imelenga kwenye maeneo muhimu huku akisema  kuwa Kuna haja  ya kuboresha fani ya ufundi na makazi  ya wafanyakazi wenye pato la chini akitolea Mfano wa nchi ya Singapore ambayo imeboresha makazi ya wafanyakazi na kuchangakia kuongeza pato kwa serikali.

No comments