SADAKA Network Kuweka Kambi Ya Uchunguzi Waathirika Wa Matukio Ya Kikatili Ili Wafanyiwe Upasuaji Kisarawe
Shirika la SADAKA
network linataraji kuwa na kambi ya uchunguzi kwa mara ya kwanza wilayani
Kisarawe Mkoani pwani ikilenga kuwatambua wagonjwa wenye uhitaji wa upasuaji wa
kuboresha maumbile kwa awamu ya 5 utakaofanywa na Hospitali ya Aga khan
kushirikiana na Muhimbili.
Akizungumza na
waandishi wa habari Meneja Miradi wa Shirika hilo Viola Julius amesema kuwa
kambi hiyo itafanyika hospitali ya wilaya ya kisarawe Juni 29 na mganga mkuu wa
wilaya hiyo atakuwepo ambapo wanawake na watoto wenye ulemavu mbalimbali
unaotokana na kufanyiwa vitendo vya kikatili majumbani watahudhuria ili
kufanyiwa tathimini ya awali na wataalamu.
Aidha ameongeza
kuwa upasuaji huo wa kuboresha maumbile, ngozi iliyokakamaa umeonyesha
kuboresha kwa kiwango kikubwa maisha ya wale wanaosumbuliwa na unyanyapaa na
ulemavu kwa kurudi katika hali yao ya kawaida na kufanya shughili za
kimaendeleo.
Hata hivyo Programu
hii ilianzishwa mnamo Januari 2016 ikihusisha wapasuaji kutoka Marekani, Canada
na Ulaya wakifanya kazi kwa karibu na wanatiba wa Kitanzania ambapo Hadi Sasa
operesheni 143 za upasuaji zimefanywa bila gharama yoyote kwa wagonjwa ambao ni
wahanga wa ukatili wa majumbani, kuungua na ajali na kurejesha utendaji wa
kimwili na mwonekano wa wanawake na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
No comments