Breaking News

TMA YAWAKUMBUSHA WANAHABARI KUWASILISHA KAZI ZAO TUZO ZA WANAHABARI BORA WA HABARI ZA HALI YA HEWA

Dar es Salaam - "Mamlaka ya hali ya hela Tanzania (TMA) inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha warsha za wanahabari zinaendelea kuwa endelevu na kuboreshwa zaidi, Hatua za uboreshwaji ni pamoja na uanzishwaji wa Tuzo za Wanahabari bora wa habari za hali ya hewa kila mwaka, hivyo ninawakumbusha wanahabari wote nchini, kuwasilisha kazi zenu za ushindani kupitia barua pepe elekezi ili muda wa mchakato ukifika wapatikane washindi waliokidhi vigezo.” 

Hayo yalizungumzwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alipokuwa akifungua rasmi mkutano wa wanahabari katika kujadili Utabiri wa Mvua za Msimu wa MASIKA unaoanzia mwezi Machi hadi Mei 2025. 
Aidha, Dkt. Chang’a aligusia kuhusu changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuwa mwaka 2024 ulivunja rekodi kwa kuwa mwaka wenye ongezeko kubwa zaidi la joto Duniani kwa ongezeko la takribani nyuzi joto 1.550C na upande wa Tanzania ongezeko la joto lilifikia nyuzi joto 0.70C, hivyo kuashiria uhitaji wa jitihada kubwa za pamoja za jumuiya ya kimataifa za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Aliwahamasisha wanahabari kujipanga vizuri ili kuendelea kuelimisha jamii. 

Kwa upande wa mwakilishi wa wanahabari kutoka Daily News Digital Bi. Zaituni Mkwama alitoa mrejesho wa namna walivyosambaza Utabiri wa mvua za Vuli 2024 uliotolewa na TMA kwa kuonesha kuwa mvua hazitakuwa za kutosha, hali iliyosaidia Serikali kuweka miundombinu mizuri na kuhakikisha chakula kinapatikana cha kutosha hapa nchini. 
“Baada ya wanahabari kusambaza Utabiri wa Mvua za VULI 2024 uliotolewa na TMA ilipelekea Serikali kuweka miundombinu rafiki kwa kuhakikisha chakula kinapatikana kwa kuitosheleza nchi.”. Alisema Bi. Zaituni Mkwama. 

Katika mkutano huu, wanahabari walipata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei, 2025 na kutoa michango yao juu ya namna bora na sahihi zaidi ya usambazaji wake.

No comments