Hatua Kali Kuchukuliwa Kwa Wanaoghushi Vyeti Kuingia JKT.
Jeshi la Wananchi
wa Tanzania JWTZ limesema kuwa usaili unaoendelea kote nchini wa uandikishaji
wa vijana JWTZ/JKT watafanya uhakiki upya wa vyeti na nyaraka zote za vijana
walioandikishwa baada ya kubainika uwepo wa udanganyifu katika taarifa zao.
Akizunguma Jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari Jeshini Luteni Kanali Gervas Ilonda
ambapo amesema katika zoezi la uhakika watashirikiana na NIDA, Baraza la
mitihani ili kwabaini walio toa taarifa za uongo kukamatwa na kuchukuliwa hatua
za kisheria.
Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza kwenye zoezi hilo ni pamoja vijana kwenda
kujiandikisha kwenye mikoa mingine hivyo kuwanyima fursa wengine kwani kila
mkoa umepewa nafasi yake kulingana na idadi ya watu.
Luteni Ilonda aliongeza kuwa
baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwaombea ndugu/ jamaa zao nafasi za kujiunga na
JKT jambo ambalo ni kinyume na utaratibu huku vijana wakitoa taarifa za uongo
ikiwemo kughushi vyeti vya kuzaliwa na vile vya elimu jambo ambalo ni kosa la
jinai.
“Vijana wengi
wamebainika kutoa taarifa za uongo ili kujipatia nafasi na wengine kufanya
vitendo viovu vya kushawishi na kujaribu kutoa rushwa na hatimaye kughushi
vyeti vya kuzaliwa na vile vya elimu, hii ni kosa la jinai yeyote anayebainika
atachukuliwa hatua za kisheria”Amesema Luteni Kanali Ilonda.
Alisema Kuna baadhi
ya watu wasio waaminifu huwarubuni vijana vijana na wazazi kuwataka watoe fedha
ili waweze kuiingizwa JKT hivyo wanapokutana na watu kama hao watoe taarifa kwa
mamlaka husika kwani Jeshi halidai Fedha zozote bali Ni kufuata taratibu
zilizowekwa.
Nitoe rai wananchi kutoa taarifa za watu wanaowahisi kuwasaidia vijana hao
kufanya udanganyifu ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na vijana kutambua
kuwa Jeshi hilo halitoi ajira bali ni mafunzo ya kuwajengea umoja wa kitaifa,
Mshikamano, maadili mema, uzalendo na stadi mbalimbali za kujitegemea.
No comments