Rais Magufuli: Uzeni Gesi Msiuze Mitungi
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara na
wauzaji wa gesi nchini kuuza bidhaa ya gesi tu na sio mitungi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ghala la mitambo ya kuchakata gesi iliyoko Dar-es-salaam, Wilayani ya Kigamboni, Rais Magufuli amesema kuwa sekta binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi nchini na kuwahakikishia kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana nao.
“Nimefurahi kuona Taifa Ges mmeanza kukarabati na kutengeneza mitungi yenu wenyewe hii itashusha bei ya mitungi na kuwawezesha wananchi wengi kutumia gesi, tena kwa hii ikiwezekana fanyeni kama makampuni ya soda na bia’’, Alisema Rais Magufuli.
Akisisitiza jambo hili Rais Magufuli ametoa mfano wa Kampuni za Soda na Bia ambapo ukinunua soda na bia maana yake hulipii creti ila unalipia soda hii itasaidia kupunguza bei ya gesi na kuwafanya wananchi wengi kutumia nishati hii
Rais Magufuli amewataka wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000.
“uwekezaji huu mkubwa uliofanywa na Taifa Gas Ltd ni uthibitisho, Serikali yetu inaipenda sekta Binafsi na ipo tayari kushirikiana na ninyi, kwa hiyo Sekta Binafsi endeleeni kujiamini, endelezeni kazi pamoja, hapa Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji”, Rais Magufuli.
Rais Magufuli alisema kuwa Tanzania inahitaji wawekezaji muda wote ili kuwekeza katika sekta ya nishati kama vile kuzalisha umeme utokanao na Makaa ya mawe, Maji, Upepo pamoja na Jua ili kuwezesha upatikanajiwa umeme wa kutosha na kwa bei nafuu.
“Wawekezaji tuwahitaji leo, kesho, kesho kutwa na miaka yote, kwa sababu Tanzania ipo miaka yote, kwa hiyo wawekezaji na ninyi tunawahitaji kwa sababu tutakusanya kodi na watanzania watapata ajira kama ambavyo Taifa Gas mmefanya”, Alisisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia aliwataka wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000.
Naye Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani alisema kuwa biashara ya gesi sasa imeendelea kukua nchini tofauti na hapo zamani ambapo kwa sasa gesi inafika hadi vijijini.
“Biashara hii ya gesi imekwenda hadi kwenye baadhi ya mikoa, naipongeza na kuishukuru kampuni ya Taifa ya gesi, ambayo kwa afrika ina maghala makubwa na kuhifadhi na kupokea gesi kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, kwani wanahifadhi tani 7,650, wakifuatiwa na Afrika ya Kusini tani 5,200 huku Morocco wakihifadhi tani 5,077 kwa hiyo sisi ni namba moja”, Alisema Dkt.Kalemani.
Aidha Dkt.Kalemani aliongeza kuwa kwa sasa bei ya gesi imeshuka kuliko nchi zote Afrika Mashariki, kwani kilo moja ya gesi inauzwa Shilingi 3,080, kenya 3,500 huku Uganda ikiuzwa kwa 4,001.
Dkt.Kalemani alisema kuwa Sekta ya gesi imepunguza changamoto ya ajira kwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 12,000 katika kampuni za gesi zilizowekeza nchini.
Biashara ya gesi nchini ilianza mwaka 1965, huku kampuni ya gesi ya Tipper ilikuwa mshiriki mkuu wa biashara hiyo, ambapo gesi ilikuwa inatumika viwandani, Mashuleni, katika Taasisi za Serikali na Vyuoni.
No comments