Mahakama Yaamuru Wema Sepetu Aende Gerezani Siku 7
Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuamuru Msanii Wema Sepetu kwenda gerezani
siku saba mpaka Juni 24 akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia
dhamana.
Nyota huyo wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono mitandaoni kupitia simu yake ya kiganjani.
Nyota huyo wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono mitandaoni kupitia simu yake ya kiganjani.
Uamuzi huo wa
Mahakama umefikiwa leo Juni 17, mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati
mshtakiwa huyo alipofikishwa mbele yake.
Wakili wa Serikali
Glory Mwenda amedai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa hapo baada ya mahakama
wiki iliyopita kutoa hati ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.
Hakimu Kasonde
alimtaka Wema kujieleza kwanini asifutiwe dhamana kwa kushindwa kufika
mahakamani kwa tarehe mbili tofauti.
Akijieleza Wema
alidai Mei 14 mwaka huu hakufika sababu alikuwa safarini mkoani Morogoro
na Juni 11 mwaka huu aliumwa akashindwa kupandisha mahakamani.
Mshtakiwa aliomba
msamaha na Wakili wa Serikali, Mwenda aliomba Mahakama impe onyo mshtakiwa ili
asirudie kufanya kitendo hicho chenye usumbufu.
Hakimu Maira
alisema kasikia hoja zilizowasilishwa na atapitia kiapo cha mshtakiwa kisha
atatoa uamuzi Juni 24 mwaka huu na akaamuru katika kipindi cha kusubiri uamuzi
mshtakiwa akae rumande.
Wema anadaiwa
kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya
Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa hazina maudhui.
No comments