Katibu Mkuu CCM Dr. Bashiru Ahoji Maswali Haya Kwa Wanaosema Uchumi Wa Tanzania Haukui
KATIBU wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM)Taifa ,Bashiru Ally amezindua ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa
mikutano wa CCM mkoani Pwani,ambapo amechangisha zaidi ya milioni 25 na vifaa
mbalimbali.
Katika uzinduzi
huo, jumla ya mifuko ya saruji 2,861 imechangiwa ,nondo tani tano thamani ya
milioni 9 ,malori ya mchanga, fedha taslimu ni sh.milioni 22.562 na ahadi ni
sh.milioni 2.5 .
Alisema kati ya
fedha hizo milioni tano imechangiwa na mwenyekiti wa CCM Taifa dk.John
Magufuli.
Bashiru alisema, kwasasa
hakuna mtindo wa kuchangia shughuli za kichama kwa fedha za mikononi ili kuweka
mifumo mizuri ya kuaminiana.
Aidha alisisitiza
ujenzi wa ofisi za chama ili kukijenga chama kwa maslahi ya wanaCCM.
“Uhai wetu
unatokana na vikao na vikao haviwezi kufanyika chini ya miti,au kukutana gesti
,hivyo jengeni ofisi za chama kuanzia matawi na kata ili kuimarisha chama
chetu”
Hata hivyo
aliwasihi wananchi wasiwasikilize wale wanaokebehi Chama kilichopo madarakani
na wale wanaopotosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.“Upotoshaji ni dhambi hasa
kwa mtu aliyesoma chuo cha Dar es salaam na kusisitiza kwamba ,hali ya uchumi
wetu ni imara” .
“Huwezi kudanganya
watu na kuwaona ni wa pumbavu ,hakuna uchumi uliokufa ,hatuna deni la
ndege,tunajenga vituo vya afya ,tunatundika nishati ya umeme hadi
vijijini,watoto wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne leo
mtu unaibuka anasema uchumi umekufa”alikemea Bashiru.
Hakusita
,kuupongeza mkoa kwa kushirikiana ,kushikamana na kuwa na mahusiano mema baina
ya serikali na chama. Aliweka wazi wilaya ambazo bado hazina mahusiano mazuri
kati ya serikali na chama ikiwemo Bagamoyo ,Rufiji na Kibaha Vijiji ambako pale
tatizo lipo kwa mkurugenzi mtendaji wa Kibaha Vijijini.
Alimjia juu
mkurugenzi huyo wa wilaya ya Kibaha kwa kufanya kazi zake kwa mazoea na
kushindwa kujenga mahusiano na ushirikiano na chama na kwenye majukumu yake ya
kazi. Katika hatua nyingine akielekeza juu ya muelekeo wa chaguzi zijazo
,Bashiru aliwataka viongozi wanaokaa kwenye vikao vya maamuzi waache kutembea
na wagombea mifukoni na badala yake waache wabunge,madiwani na wenyeviti wa
serikali za mitaa waliopo wafanye kazi.
Pia aliwaasa baadhi
ya wabunge kuacha kutumwa na kuwa wapiga debe kwa wawekezaji uchwara bali
waelekezeni wawekezaji masharti na taratibu za nchi kwa maslahi mapana ya nchi.
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
No comments