UVCCM Tawi la Chuo Cha DMI Wafanya Kongamano La Kuajadili Utekelezaji Wa Ilani Ya Chama Jijini Dar.
Umoja wa vijana wa
chama cha Mapinduzi tawi la chuo kikuu cha mabaharia DMI umeiomba Serikali
kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabali chuo hicho ikiwemo
kuwapatia vitendea kazi kama vile Meli ili kuwawezesha kufanya mafunzo
kwa vitendo baada ya kuhitimu masomo yao.
Akizungumza Jijini
Dar es salaam katika ufunguzi wa kongamano la kujadili utekelezaji wa
Ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa
Vyuo Vikuu nchini ambaye pia mwenyeketi mstaafu wa Tawi hilo Bw.Tahilisu Mnali
alisema pamoja na Taaluma hiyo ikitumika ipasavyo inaweza kuwa na mchango mkubwa
kwa taifa.
“Chuo kimekuwa
kikitoa wahitimu walio na viwango vya kimataifa ila nitoe rai kwa serikali
kusaidia kutatua changamoto ya vitendea kazi kama vile meli ili kuwawezesha
wahitimu hao pindi wanapoitimu masomo yao waweze kuwa na sehemu ya kufanyia
mazoezi ya vitendo” alisema Bw. Mnali.
Aliesema Taaluma ya
uhandisi ina nafasi kubwa katika kuiwezesha serikali kufikia azma yake ya
uchumi wa viwanda hivyo kama wahitimu wa mafunzo ayo watapata vitendea kazi ni
rahisi kuwezesa azma hiyo ya serikali kufikiwa kwa wakati.
Mapema akizumgumza
wakati wa ufunguzi wa kongamanlo hilo mlezi wa Jumuiya ya vijana wa chama
cha Mapinduzi chuo cha DMI Dokta Benjamini Mbeba amewataka
wanafunzi kusoma kwa bidii kwani kutokana na Taaluma wanayosomea kuwa ni
miongoni mwa Taaluma mambazo ni chachu katika kuisaidia serikali kuelekea
katika azma yake ya uchumi wa viwanda.
Nae Kaimu Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Dokta Eliamini kassembe alisema sekta ya bahari ina
mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania hivyo amewataka vijana
kusoma kwa malengo pamoja na kuongeza nidhamu huku chuo hicho kikiendelea
kutafuta njia ya kutatua chanagmoto zao.
Akizungumza kwa
niaba ya wanafunzi wa chuo hicho ambae pia ni katibu wa uvccm chuoni hapo Bw.
Frank Muchunguzi alisema changamoto ya miundombinu Chuoni hapo bado
haikidhi utendaji kazi wao ikiwemo uchache wa madarasa jambo ambalo
linarudisha nyumba juhudi zao hivyo wameiomba Serikali kusaidia kutatua
changamoto hiyo.
Washiriki wa kongamano hilo wakichangia mada
No comments