Breaking News

Dkt. Mwinyi Awataka Walezi Na Wazazi Kujikita Katika Malezi Bora Ya Watoto

Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa mhe husseini mwinyi ameitaka wazazi na waleji kujikita zaidi katika malezi bora ya watoto wao kiimani na kielimu ilikuweza kuwa na taifa bora. 

Akiongea katoka kilele cha mashindano ya 3 kitaofa ya kuifadhi quan tukufu mhe mwinyi alisema ipo aja kwa wazazi na walezi kuweka msisitizo wa kwa watoto kuwaendeleza kielimu hususani mafundisho ya kidini kwa lengo la kuwajenga vijana kiimaninna kiroho..

"Nitoe rai kwa wazazi na walezi kutoa msisitizo kwa watoto wao kusoma kwa bidii na kuwa karibu nao kuweza kuwashauri na kuwapatia mafunzo jambo litakalosaidia kuwajenga kiimani ivyo kuwafanya kuwa na misingi imara" Alisema dkt Mwinyi
Alisema serikali ya awamubya tano inatambua mchango mkubwa wa taasisi hiyo katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya hivyo itaendelea kushirikiana nao hususani wizara ya elimu katika kutekeleza maswala ya kielimu.

Pia dkt Mwinyi amewataka waislam na wengine nchini kuendelea kudumisha amani, umoja na msikamano uliopo nchini kwani ni moja ya tunu ambayo tumejaaliwa na mwenyezi Mungu ivyo tuilinde na kuidumisha.
Mapema akiongea wakati akimkaribisha mgen rasmi shekh Seif Bin Ally Seif kutoka taasisi ya Istiqaama Muslim Community of Tanzania alisema mashindano haya ya kuifadhi Quan tulufu yanafanyika kwa mara ya 3 kitaifa wakati kikanda ni mara ya 9 yenye lengo la kuwawezesha vijana kuonyesha uwezo wao wa kuifadhi quan tukufu.

Alisema pia taasisi hiyo imekuwa mstali wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii kama ujenzi wa Shule na vituo vya afya kwa lemgo la kusaidia juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais magufuli kuwaletea maendeleo wananchi.

No comments