Mmiliki Wa First Supper Market Bi Devota David Ashinda Tuzo Ya Mafanikio Makubwa Ya Thamani Ya Mwanamke Na Ajira Binafsi Jijini Dar.
MJASIRIAMALI Devota David ambaye ni mmiliki wa First
Supper Market iliyopo mbezi beach kona ya Goba akipokea Tuzo ya mafanikio
makubwa ya Thamani ya Mwanamke na ajira binafsi katika hafla iliyofanyika
ukumbi wa king solomoni jijini dar es salaam.
Pichani ni Tuzo ya mafanikio makubwa ya Thamani Ya Mwanamke Na Ajira Binafsi
Mmiliki First Supper Market Bi, Devota David.
Na Francis Peter
MJASIRIAMALI Devota David ambaye ni mmiliki wa First
Supper Market iliyopo mbezi Mbeach kona ya Goba Dar es Salaam amefurahia kupewa
tuzo ya mafanikio makubwa ya Thamani ya Mwanamke na ajira binafsi katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomon Jijini Dar es saaam.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo ilianza rasmi kutolewa nchini mwaka 2017 kwa
malengo ya kutambua na kazi za za jamii ya wanawake nchini Bi Devota alisema
nafuraha kubwa kufanikiwa kwangu nimeweza kutambulika kama mwanamwake niliyejiajiri na Kazi zangu
kutambulika kwa jamii.
“Nashukuru wote
waliwezesha siku ya leo kupata tuzo hii yenye lengo la kuipa thamani Ajira
binafsi sawa na Ajira rasmi ambayo inachukua kiasi kidogo cha wanawake
kulinganisha na ajira binafsi” alisema bi Devota.
Alisema Tuzo hiyo kwake ambayo itamsaidia kumjengea
ujasiri wa kuendeleza mapambano ya mafanikio na sasa ataweza kufanikiwa zaidi
kwani maadhimio ya mafanikio yake hayo atayazidisha kwa bidii ili kuzidi
kung'ara baada ya kongamano hilo.
Aidha Bi devote amewashauri
waandaaji kuendelea kufanya Kongamano
hilo
Kwani kufanya hivyo
kuwawezesha wanawake zaidi kuwa na hali ya kujiamini zaidi katika kazi
wanazofanya hivyo kutakuwa na mafanikio
makubwa yaliogusa maisha ya wanawake wa Tanzania.
"Nawaombe
wanawake wenzangu waliojiajiri kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kufanya
maandalizi ya kukutana na wanawake wengine Siku nyingine tena ambapo historia
itajiandika tena," alisema Bi.Devota.
Akielezea namna
alivyoweza kuendesha biashara zake kwa muda mrefu mpaka kufikia hapo ilopo na
kupata mafanikio alisema ni kujituma na kuwa na ubunifu zaidi kwa kile
unachofanya pamoja na anajivunia kupata sapoti zaidi kutoka kwa mumewe.
"Nikiwa katika
mazingira ya utoto zamani nilianza kuwa namsimamia mama yangu mzazi pindi
nikitoka shule niliachiwa biashara na mama, mama alikuwa akimili depo moja
niliweza,"alisema Devota.
Anasema hivyo
kutokana na kuanza mapema mazingira hayo aliyokuwa akimuona, alianza kupenda ajira
za kujiajiri, ambapo kwa sasa taswira ya serikali ya awamu ya tano inapigania
vipao mbele katika ajira za wajasiriamali binafsi.
Mwonekano wa baadhi
ya bidhaa zinazo patikana First Supper Market iliyopo mbezi Mbeach kona ya Goba
Dar es Salaam.
Mmiliki wa First
Supper Market Bi, Devota David akiwa katika picha ya pamoja na wenzake mara
baada ya kupokea tuzo zao, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa king solomoni
jijini dar es salaam.
No comments