Breaking News

RUNGWE: Awashukia Viongozi Wanaotumia Nasafi Zao Kumshambulia CAG.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini Mhe Hashim Rungwe ameelezea kusikitishwa kwake kwa kauli za viongozi waandamizi ambazo wamekuwa wakizitoa kwa mkaguzi na msimamizi wa hesabu za serikali nchini Profesa Mussa Assad.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juu ya mambo mbalimbali yanaendelea nchini alisema sisi kama taifa sasa tunaelekea kubaya kutokana na kukisili vitendo visivyo vya kimaadili wazi ikiwemo azimio la bunge la kutokufanya kazi na CAG.

"Kama taifa tumetoka katika misingi yetu ya jambo ambalo linaweza kusababisha kuwa nchi isiyotawalika, isiyofaa misingi ya utawala bora, uwazi uwajibikaji na demokrasia ambayo tumekuwa nayo miaka mingi" Alisema mhe Rungwe.

Alisema kiongozi apendi kukosolewa au kuambiwa ukweli kuhusu namna ya utendaji kazi wake jua kuwa kuna tatizo katika utendaji wake na maamuzi yake pia.

"Kiongozi yeyote mwenye busara yafaa uwe na uvumilivu, usikivu, hekima na busara jambo ambalo litasaidia kuwa na fikra chanya, mawazo endelevu kutoka kwa watu wake wa karibu na sio kutumia cheo chake kumuadhibu mtu kwakuwa tu amekosoa au amerekebisha jambo" Alisema mhe Rungwe.

Mhe Rungwe aliongeza kuwa Watanzania ndio wamekuwa wakitumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu wakati ndie mkaguzi wa kodi zetu, ivyo kuamua kusimama nae.

No comments