Breaking News

LHRC Yazindua Mfumo Wa Kidigitali Wa Kukusanya Taarifa Za Haki Za Binadamu Nchini

Image result for mkurugenzi wa lhcr anna henga
Kituo cha sheria na Haki za binadamu kimezindua mfumo mpya wa kidigitali wa kukusanya taarifa mbalimbali za haki za binadamu zinazotokea maeneo mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo serikali, jeshi la polisi kwa lengo la ufuatiliaji zaidi wa ulinzi na haki za binadamu nchini.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mfumo huo mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Bi Anna Henga alisema mfumo huo wa kidigitali upo kwa njia ya kisasa na rafiki kwa watu wote ambapo wananchi wanaweza kuripoti hasa wale waliopo katika maeneo magumu kufikia kama vijijini.

"Kupitia mfumo ambao utatoa fursa kwa wananchi hususani waliopo vijijini kutoa na kuripoti tukio lolote la uvunjifu wa haki za binadamu kupitia tovuti (website), Simu za mkononi zinazotumia App za smartphone kwa mfumo wa Android na IOS sambamba na kutuma ujembe wa maneno kwenda namba +255699695486" Alisema Bi Henga.

Alisema mfumo huo utasaidia kupunguza changamoto kubwa ya utolewaji taarifa za haki za binadamu hasa kwa wananchi, walinzi na watetezi wa haki za binadamu waliopo katika maeneo magumu kufikia.

Katika hatua nyingine akizungumzia kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo inaadhimishwa leo duniani bi Henga amevitaka vyombo vya habari nchini kudumisha misingi imara ya sekta ya habari kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari nchini.

"Ni vema jamii ikatambua misingi ya uhuru wa habari ili kulinda na kuzuia mashambulio dhidi ya wanahabari pamoja na kuenzi wanahabari waliokuwa na mchango wa kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya vyombo vya habari" Alisema Bi Henga.

No comments