RC MAKONDA Apongeza Watendaji Kwa Kufanikisha Jiji La Dar Kuibuka Kidedea katika Makusanyo Ya KODI.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewamwagia sifa wakurugenzi wa Halmashauri na watendaji kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa Mapato*jambo lililopelekea Dar es salaam kuibuka namba moja kitaifa katika Makusanyo ya mapato katika Robo ya Mwaka.
Mkoa wa Dar es salaam umeibuka kidedea kwa kukusanya kiasi cha silingi Bilioni 118.4 ukifuatiwa na Mkoa wa Dodoma uliokusanya Shilingi Bilioni 57.3 huku wilaya ya iliyoongoza kitaifa ikiwa ni Ilala ikifuatiwa na Kinondoni pamoja na Temeke iliyoshika nafasi ya Tatu kitaifa.
Aidha RC Makonda amewahimiza Watendaji kuendelea kusimamia vyema makusanyo ya kodi pasipo kuwabugudhi wananchi ili kuwezesha Mkoa huo kuendelea kushika *namba moja.

No comments