Mhe Makamba: Serikali Kuandaa Sera Kurasimisha Shughuli Ukusanyaji Taka
Serikali imesema ipo haja ya kuirasimisha shughuli inayofanywa na watu ya kuokota chupa za maji ili iwe ajira rasmi kutokana kazi hiyo kuasaidia kupunguza uchafu.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu Rais muungano na Maazingira mhe,January Makamba wakati akifungua wa mkutano wa kimataifa wa Mtandao wa wasakataji na usimamizi wa mazingira ulioandiliwa chuo Kikuu cha Dar Es Salaam shule kuu ya Biashara(UDBS) alisema Halmashauri nchini zimekuwa zikitenga mpaka asilimia 20 ya bajeti yake kwa ajili ya kukusanya taka nchini.
"Pamoja na halmashauri kutumia mpaka asilimia 20 ya bajeti yake ukusanyaji wa taka pamoja uchakataji wa taka bado kumekuwepo na changamoto nyingi hususani ukusanyaji wa taka hizo" Alisema Mhe Makamba.
Alisema kwa sasa majiji mbali mbali hapa nchini yameelemewa na takataka huku akisema kitendo wanachofanya watu wanaokota chupa za maji ya kwa ajili ya kwenda kuziuza wanafanya kazi nzuri ya kusaidia kupunguza tatizo la uwepo taka .
"watu wanaofanya kazi hizo wakati mwingine wanaonekana watu wenye ugonjwa wa akili kutokana na kupita kwenye maduka au majumbani kwa watu lakini kazi wanayofanya ni ya kuongeza kipato hivyo serikali inaona umuhimu wa kuilasimisha kazi hiyo kuwa rasmi" Alifafanua mhe Makamba.
Aidha mhe Waziri Makamba amezitaka taasisi za serikali pamoja na vyuo kuongeza kufanya tafiti ambazo zitaweza kuleta fursa za kuzifanya takataka kuwa sehemu ya kuongeza kipato kwa taka hizo.
Nae Mratibu Msaidizi wa mkutano huo kutoka chuo Kikuu cha Dar Es Salaam shule kuu ya Biashara (UDBS) Dk Nelly Mallima alisema katika mkutano huo washiriki watajadili jinsi ya kuweza kuondokana na taka pamoja kuzichakata na kuwa fursa ya kuongeza kipato.

No comments