Kampuni Ya CDS kwa Kushirikiana Na Kampuni Ya Godel Yazindua Mfumo Mpya Wa Ufuatiliaji Mizigo Mtandaoni
Hussein Ndubikile
Kampuni ya Usafirshaji wa Mizigo na Vifurushi ya CDS kwa kuingia ubia wa ushirikiano na Kampuni ya Godel kutoka Uingereza imezindua Mfumo mpya wa teknolojia ya usafirishaji mizigo kwa ufuatiliaji wa mtandaoni.
Akizindua mfumo huo wa kisasa jijini Dar es Salaama Meneja Mkuu wa kampuni ya CDS, Juma Uledi amesema kampuni hiyo ina miaka 15 tangu ianzishwe na kwamba kutokana na mabadiliko ya makubwa ya teknolojia wamaeona umuhimu wa kuingia ushrikiano na kampuni ya Godel lengo likiwa kutoa huduma bora kwa wateja wao.
"Kampuni ina miaka 15 inatoa huduma ya usafirishaji tumeona mfumo wa analojia una changamoto nyingi tukaona tushirikiane na Godel tunaamini mfumo ambao umezinduliwa unakwenda kuongeza ufanisi wa utoaji huduma," amesema Uledi.
Amebainisha kuwa Kampuni ya Godel inafanya vizuri shughuli za usafirishaji kwa mfumo nchini Uganda na kwamba mizigo itatakayosafirishwa itawekwa kitufe maalum kitakachokuwa kikionyesha mahali ulipotoka na mahali unapokwenda kwa usalama wa uhakika.
Amesisitiza kuwa mfumo huo ni rahisi kimatumizi kwani mteja ataweza kufuatilia mzigo au vifurushi vyake kwa kutumia simu yake ya mkononi hivyo itakuwa rahisi kujua uendapo na endapo utapata changamoto yoyote
Amefafanua kuwa kuanza kwa mfumo huo kutasaidia kufungua fursa za ajira kwa vijana katika mikoa yote ambayo CDS inatoa huduma zake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CDS, Masoud Wannani amesema mfumo rafiki ambpo mteja yeyote mwenye kumiliki simu janja (Smartphone) anaweza kufuatilia mzigo wake ili mradi simu yake iwe imeunganishwa kwenye mtandao (Internet).
Masoud amesema wameamua kuzindua mfumo huo kwa kushirikiana na kampuni Godel kwani kampuni hiyo ina uzoefu na TEHAMA huku akisistiza katika miaka 15 ya ufanyaji kazi wamepata wateja hivyo wamekuwa wakibaliana na changamoto ya upotevu wa mizigo au kuchelewa.
Kwa upande wake Muasisi wa Kampuni ya Godel, Paresh Chandarana amesema wana uzoefu wa miaka 35 ya utoaji huduma ya usafirishaji wa mizigo katika nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza na kwamba anaamini mfumo huo ni suluhisho la kuwapunguzia adha wateja waliyokuwa wakipata awali ndio maana wakaamua kuuleta Tanzania.
Naye Mtalaamu wa masuala ya teknolojia ya mwasiliano wa kampuni hiyo, Shallin Ghelan amesema kuwa wana ofisi katika nchi ya Uganda na kwamba mfumo huo utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakizipata wateja.
No comments