Mchungaji Mashimo Atamka CAG kuomba Radhi Na Kufanya Toba Kutokana Na Kauli Yake Ya Bunge Ni Dhaifu
Mchungaji wa Manabii na Mitume Komando Mashimo amemtaka Mkaguzi wa hesabu za serikali nchini Prof. Mussa Assad kuomba radhi kufatia kauli aliyoitoa kuwa Kuwa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dhaifu.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam mchungaji mashimo alisema ueleweke kwamba bunge ni takatifu ivyo bunge aliwezi kuwa dhaifu bali baadhi ya wabunge waliopo ndani ya bunge ndio dhaifu.
"kufatia ziara niliyoifanya bungeni na kuudhulia na kuona baadhi ya vikao vinavyoendeshwa na mijadala inayofanyika ndan ya bunge nimejiridhisha kuwa bunge sio dhaifu kama ilivyoelezwa na Mkaguzi wa hesabu za serikali" Alisema Mchungaji Mashimo.
Nitoe wito kwa mkaguzi wa hesabu za serikali nchini pamoja na wote ambao wamekuwa wakisema kuwa bunge ni dhaifu kuomba radhi pamoja na kufanya maombi ya toba kutokana na kulikashifu bunge wakati bunge ni sehemu takatifu.
Aidha mchungaji mashimo aliongeza kuwa katika kipindi chote ambacho alikuwa akiudhulia vikao vya bunge ametambua uwepo wa wabunge ambao ni dhaifu kutokana na mienendo yao bungeni.
Amemtaja mmoja ya wabunge hao ambao kwa mujibu wa maono yake kuwa ni dhaifu ni mchungaji msigwa kutokana na kuwa anapinga kila jambo akiwa Bungeni kwa kufanya hivyo tayali anadhiilisha kuwa ni dhaifu.
"Katika kipindi chote ambacho nliudhulia kuona namna vikao vya bunge vinavyoendeshwa nimejiridhisha pasi na shaka kuwa mchungaji msingwa ni mmoja ya wabunge dhaifu kutokana na kupinga kila hoja ina miswada inayowasiswa bungeni" Alisema Mchungaji Mashimo.
Pia mchungaji Mashimo amewapongeza wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana wanavyotekeleza majukumu yao hususani wa chama cha mapinduzi ccm kwa kipindi chote wawapo bungeni..
No comments