Breaking News

Majina Ya Viongozi Wa Jumuiya Walioteuliwa Na Profesa Lipumba.

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amefanya uteuzi wa makatibu watendaji wa Jumuiya zote za Chama ambao wataratibu na kusimamia  kukamilisha uchaguzi za jumuiya zote za chama. Kwa kipindi cha miaka 5.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari ametaja Jumuiya ya vijana wa CUF amemteua Mhe Hamidu Bobali kuwa kaimu mwenyekiti wa jumuiya hiyo, makamu mwenyekiti ni Faki Suleman Khatib, mhe Yusuph Kaiza Makame ameteuliwa kuwa katibu Mtendaji, naibu wake ni Mbaraka Ismaili Chilumba.

Kwa upande wa Jumuiya ya wanawake wa CUF amemteua Mhe Dhifaa Mohamed bakar kuwa mwenyekiti, makamu mwenyekiti ni Mhe Kiza Husein Mayeye, katibu Mtendaji mhe Anna Ryoba Paul na naibu wake ni Mhe Leila Jabir Haji.

Pia profesa Lipumba amefanya uteuzi katika Jumuiya ya wazee kwa kumteua Mzee Chunga Kuwa kaimu Mwenyekiti, Bi. Hamida Abdallah kuwa makamu mwenyekiti, Hamis Hasani Mkapa kaimu katibu Mtendaji na Saidi Ali Salimu kuwa kaimu Naibu katibu Mtendaji.

No comments