MTOLEA Ajitambulisha Rasmi Kwa Wanachama Wa CcmTemeke
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRtoPZQ2h4s5rGcfec93kJrFvJNwsl5akH4-EWn851lGss6FvdyHJz3HqBeFD0Th6x9uC_Kfx-moZoMY4BWjXJvH5Ao2-BRmOzEY-yrvPMrrRDP31GtUA8WKZG_FVaV5wN9hMeWBvMSioF/s640/FB_IMG_1553873648413.jpg)
Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es salaam Mhe Abdallah Mtolea amesema atahakikisha anaendelea kushirikiana na wanachama wa CCM pamoja nawananchi wa jimbo lake la Temeke ili kuendelea kutekeleza ilani ya chama hicho.
Akizungumza katika hafla ya kujitambulisha kwa wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema amefanya hivyo kutokana na kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo wa marudio baada ya kujiengua Chama cha wanachi CUF na kuhamia CCM.
"Nipo hapa leo na kukutana na viongozi kutoka ngazi mbalimbali wa chama cha mapinduzi ccm zaidi ya 1200 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi sambamba kujadiliana, kushauliana na kupanga mikakati juu ya utekelezaji wa ilani ya chama". Alisema Mhe Mtolea.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgL77-btcS4iYMUijEqyiP3S7UKl1W4vtTrKfqEwGUL3vzN8d2qfyHd2O2U2jWXYDcbn9GOk3uBmnATrSglza3KNZvw7pTLqvj1PU_pHrrBpJK2Rcz_JqUt9PqbhWUrJFuuMTFFktSaqn6A/s640/IMG_20190329_122202.jpg)
Alisema kupitia mkutano huo pia watajadiliana utekelezaji wa ilani ya chama pamoja na namna ya kutatua changamoto zilizopo jimboni hapo hususani ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami ambapo alibainisha kuwa zaidi ya Bil 265 zitatumika katika kuhakikisha suala la hilo litakuwa historia.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbe_sLF0utvEOKuMd58Z6ixWqpdG6Td-SFxhAe0wCzvANRF7cJ9WLjD8O4tgWruUqXVCuR-FAPeGSslXHgHAxS0j1J9lmAHtb0wjZvrdlIoOD3eHq6itKouRuerQ_SqGe1cL8_Ks5Q1ACH/s640/IMG_20190329_122215.jpg)
Pichani ni Baadhi ya Wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Manispaa ya Temeke jiji la Dar es salaam wakifuatilia mkutano.
No comments