Mhe Majaliwa Azitaka Halmashauri kutenga Bajeti Dhidi Ya Ukatili Wa Kijinsia.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXY2Sarv7JwQRbxIURC_WzWTBNA9KwU6MoPAWH_eodIphGtllo6wpRb3gK8kjf7VwfOwxKSuIRhDViGp_gmH4RFjmN_ALC1aUrIRgnM4ojZx0w5ylbvBhX4xfKiMEEOafDDPPg7brvskZt/s640/Screenshot_20190321-143631.png)
WAZIRI mkuu Mhe Kassim Majaliwa Amezitaja taasisi zisizo za kiserikali kuungana pamoja katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam mhe. Majaliwa alisema serikali tayali wamshazielekeza Halmashauri na mikoa zipange bajeti za kuimarisha kampeni za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
"Serikali imeshatoa mwongozo na utaratibu kuunda kamati za kushughulikia matukio hayo kwa kuziagiza Halmashauri na mikoa zipange bajeti za kuimarisha kampeni za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto" Alisema mhe. Majaliwa.
Alisema mwongozo huo utatoa utaratibu wa usimamizi na ufuatiliaji kuhusu uundwaji wa kamati mbalimbali za mfumo wa mawasiliano na uwasilishaji wa taarifa jambo litakalosaidia kuwezesha kampeni ya utoaji wa elimu kwa jamii dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPIe8Tx8Q78hJ78CndvilqFlBX4wfi9z0jJZk0eypy7z8p535j183KeWeVsXO63WgbRUYkiq9rv_d935BN-EhxyF8CZYMx2ssPNPo0Jnm-526p9FP3DpbC0ovmTeHXmOGU03eonHTTTREY/s640/Screenshot_20190322-072456.png)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.
"Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto na makundi kengine unatokomezwa na haki zote zinalindwa na kuheshimiwa" Alisema mhe. Majaliwa.
Aidha Mhe Majaliwa aliongeza kuwa kutakuwa na kamati za kijinsia na ustawi wa wanawake na serikali Inaunga mkono na kutambua jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na ndoa za utotoni ikiongozwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa mtoto (CDF).
“Suala la ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni jambo mtambuka na linahitaji ushilikishwaji wa wadau katika kutokomeza janga hili linaloikabili nchini yetu.” Alisema mhe. Majaliwa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwaFi0plHIdJqdzWMc0eoswEPeKFfCGMeJvZih4_QdAqVFWTfXIUK08tzbbNlA5AJUil8QtCN58GvMBx_jUtZrDuStjsUmy0tV68yvlo7V-ky7apqA3Ut5V83lFUHsZm-v9-3C4LIxWOql/s640/Screenshot_20190322-071953.png)
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), bw. Koshuma Mtengeti akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF), bw. Koshuma Mtengeti ameiomba serikali kutoa ushirikiano pamoja na kutenga bajeti ya kutosha katika kuendesha mikakati ya kupinga ukatili wa kinjisia nchini.
"Matukio ya ukatili wa kingono bado ni changamoto kubwa nchini ambapo Mwezi Mei mwaka 2018, mwalimu wa shule ya msingi hapa jijini Dar es Salaam alituhumiwa kuwadhalilisha kingono wanafunzi wake wanne wa kike wa darasa la saba kwa kuwageuza kuwa wake zake na kufanya nao ngono,”Alisema Bw. Mtengeti.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjk1_7u9KsyFU73uUT3HudGX1-LZoVj-azNafjNCwnZepDtDTv70KSmuONJCnGCV0bqr2prel1Zs1ZzRdbEJZYj42xSs1X8FtGfnfnsO6lhQhldqJtnriRJlaFAL3j3NNZnlQxaxNkM9x5i/s640/Screenshot_20190322-072154.png)
Balozi wa USWIDI nchini Bw. Anders Sjoberg akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.
Alisema amerijika sana kutambua mchango wao unaungwa mkono na serikali na ipo nasi bega kwa bega katika kongamano hili la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mapema akiongea katika kongamano hilo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye alisema Suala la Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake ni nyanja pana, ni tatizo linalozikabili nchi zote Duniani ingawa viwango vya Ukataili hutofautiana.
Ripoti mbalimbali za haki za binadamu zimeweza kuonyesha kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha mwaka 2018 ukilinganishwa na mwaka 2017 nchini" Alisema Prof Anangisye.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuoMjV45NBM8DGiNFIgtd7NfAffN8VOVtKnzARBI0Bv7nKbyJW7G0wKetaopGEGnmZds80LVLtXyyEFcDr-Ql5qxNeYkPNnXBhabiUHVm__cHQdgAJqPCERcT6ZcNvrB_sANXQmS9Q83ef/s640/Screenshot_20190322-072549.png)
Bi Jennifer Shapke (CANADA), Akiwasilisha mada katika Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzSUbkURB0GLUZWWjTf2ctTjNKggcv0lAz2jaTD-5bIRgvAlFlz5ARUf6_BkxrVTvA4PIdGUE9bdc03SmXPJyWAk3YuTumNvFKc00Cm7UfBPuer_joJKOWE02_jHeA5AdxBLciga4ScdiR/s640/Screenshot_20190322-072114.png)
Bi Naana Otoo kutoka Shirika la FowardUk akiwasilisha mada katika Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjDbh6qBWQ9TWkQaP3_arEoDriQPvM8mCj-SmQRgQ8t2piTxUyGVwGSujmpV_iyB9vMpSGEkquB1yK1bFR60Mk5q6soGtlp03_LSFIbJrMr7UcWfRFoyQbwLMYIKbCopzecJdPqeEieWEp/s640/Screenshot_20190321-110421.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg90SmHLHoQ4WvXTFd23Y0i0uXOcIJwDGH6tXk5oEOEMoWrNmv7COCs9pyNPSakp0Q-fuDfgiuy0fzvIUXyfZtyRTr96EdqwpnV_ekW14-3vOhX1mLjnl-UCPS-mf_H1pt9e9GeCqJK8eMe/s640/Screenshot_20190321-110349.png)
Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhDhl6v0A7SEkEvFxEmOoHLEnrN2C1kpl1-CWWzEj_zLcHIFRop-bUP_4SYoH5gkFcvSJHmMRa2lQXVTuGMLcIhnzbQl4t1oot8yWIbXSw48nsE1Jk_hvEZULd2V-0d-OGMKOW_7x9YvFOa/s640/Screenshot_20190321-203444.png)
No comments