MCHANGE: Aufagilia Mswada Wa Sheria Ya Vyama Vya Siasa, Apongeza Bunge Na Serikali.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzo3T8Jv1JJbFhG3bcKgFf5Z1AHefzJUINd2EJRFVsukMWgN7NfvNPBBNmukUyl1XsUDRJliOedTkTLVYqjx8i8OaMT_UVaMGIFk7ZkcM38cfCEl742SjXjsZepeR8r2bHBp9KMJGXrHSg/s640/IMG-20190130-WA0020.jpg)
Kaimu Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Vuguvugu la Maendeleo (ADOR) Bw. Habib Mchange amelipongeza Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali kwa kuupitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw Mchange alisema pamoja na kuwepo na upotoshwaji uliofanywa na baadhi ya wachangiaji ambao walijikuta zaidi kujaribu kupotosha juu ya faida za muswada huo kwa maslahi yao binafsi.
"Taasisi ya ADOR ni miongoni mwa asasi tulishiriki katika uchagizaji wa maoni ya Muswada wa mabadiliko ya Sheria ya vyama vya siasa, tulitoa maoni kwa lengo kuwasihi watu wenye mamlaka ya Kikatiba kushiriki katika kuuandaa muswada, hivyo tunaipongeza Serikali na Wabunge kwa kuupitisha, kinachosubiriwa sasa ni saini ya rais ili kuwa sheria yenye mabadiliko," alisema Mchange.
Akielezea kuhusu upotoshaji uliotolewa na mbunge wa kawe Mhe. Halima Mdee na Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe alisema
Muswada huo ni mzuri kwani kupita kwake kunakwenda kufuta uwepo wa vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa jambo ambalo pia limepingwa na baadhi ya vyama vya upinzani.
Akijibu hoja mhe Mdee ambae alisema kuwa mswada huo unakuja ambaye anadaiwa kusema kuwa Muswada huo unakwenda kuwa Sheria inayopingana na Katiba Mchange alipinga hoja hiyo na kutolea mfano kipengele cha vyama kuwa na vikosi vya ulinzi kuwa mswada huo umekuja na majibu sahihi juu ya swala hilo.
Aidha bwana mchange ameishari serikali kutoishia kuvifuta vikundi hivyo bali iwachukulie hatua wote waliotumia vikundi vya namna hiyo katiki kukamata, kuteka na kupiga watu.
"Inapotokea kukomeshwa kwa vikundi kama hivi ni jambo la kupongeza hili, madhara ya vikundi hivi ni kwamba vimekuwa vikiwakamata, vikiteka na kuwapiga watu," alieleza Mchange.
Aidha alimpinga Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kwa hoja yake kuwa Muswsda huo kuwa utaleta Mapinduzi nchini.
Zitto jana akichangia Bungeni alitoa mfano wa aliyekuwa Kiongozi wa Ujerman Adolf Hitler ambaya mwaka 1933 alipeleka Muswada Bungeni (enabling act), wabunge wa chama chake wakaupitisha hivyo akafananisha jambo hilo na hapa nchini.
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alifika mbali na kusema kuwa hata Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano Watanzania Mwl. Julius Nyerere aliwahi kufanyiwa majaribio ya kupinduliwa kutokana na kuminya demokrasia.
Hivyo Mchange alisema kuwa hoja alizosema Zitto ni za upotoshaji na kusema kuwa ni kulikosea heshima Taifa kumfananisha Rais John Magufuli na Adolf Hitler aliyesababisha vita ya pili ya dunia huku akimtaka kumuomba radhi Mwl. Nyerere.
Aidha alifafanua kwa kusema kuwa waliotaka kumpindua Mwl. Nyerere ni Mabeberu ambapo alidai kuwa jambo ambalo hata Zitto Kabwe analifahamu lakini anashindwa kusema ukweli.
No comments