Breaking News

Chuo Kikuu Huria Tanzania na Taasisi ya kibenki ya TIOB Wasaini Makubaliano Kuboresha Taaluma.

Chuo kikuu huria cha Tanzania (OUT) wamesaini ya makubaliano ya ushirikiano kati yake na taasisi ya Wataalamu wa kibenki Tanzania (TIOB), kwa lengo la kuboresha Wanafunzi kupata juzi na maarifa kupitia raslimali za taasisi hizo.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo Jiji Dar es salaam Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Elifas Bisanda alisema ushirikiano huo ni fursa ya kipekee katika kurahisisha upatikanaji wa huduma na Vifaa mbalimbali vya kuendeshea masomo na kuleta tija kwa Taifa kutoa Wanafunzi wenye Taaluma nzuri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Mususa amesema makubaliano hayo watahakikisha Wanafunzi walio katika vituo mbalimbali wanatumia miundombinu ya TEHAMA kwa kusoma kwa njia ya Mtandao wakiwa sehemu yeyote.

Amesema makubaliano hayo ni Muhimu katika kuhakikisha kuwa wataalamu wa masuala ya kibenki wanapata mafunzo ujuzi na maarifa ya kutosha kwa maendeleo endelevu na Uchumi wa Taifa kiujumla

“Ushirikiano huo utasaidia wahitimu kuwa wabobezi na pia kuwa mwanachama wa TIOB itawawezesha kupata mafunzo kwa unafuu zaidi kwa lengo la kujenga na kuboresha huduma za kibenki katika matawi mbalimbali yaliyopo hapa nchini”Amesema Msusa.

Hata hivyo Chuo Kikuu Huria Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kisheria kwa sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992 ili kutoa elimu ya juu kwa njia huria na Masafa ambapo Chuo hicho kina mtandao mkubwa wenye matawi yapatayo 30 katika mikoa yote Tanzania bara naVisiwani. 

No comments