VIDEO INAYOSAMBAZWA NI YA MWAKA 2018 SIO YA SASA - RC KIHONGOSI
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Kenani Kihongosi ametolea. Ufafanuzi taarifa iliyosambaa katika Mitandao ya kijamii kuhusu Shule ya Budala Bujiga B ambayo ilionyesha wanafunzi wanakaa chini.
Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa Video hio ni ya mwaka 2018 na Tangu alipoingia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan madarasa katika Shule hio yalishajengwa pamoja na fedha za Madawati zilitoleea na kwasasa hakuna upungufu wa aina yoyote katika Shule hio.
Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa kujenga shule mpya Ikiwemo Simiyu Girls ambayo imeshakamilika na wanafunzi wanasoma.
Pia ameeleza wamepokea fedha zaidi ya bilion 4 za ujenzi wa Shule mpya ya Wavulana ambayo inajengwa Katika Wilaya ya Bariadi,pia ujenzi wa Shule katika kata unaendelea kwa kasi kubwa.
Hivyo amewaeleza wananchi kuzidi kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo na amewaasa wananchi Habari potofu zinarudisha nyuma maendeleo kwani hazina nia njema katika ustawi wa maendeleo ya wananchi.
No comments