Breaking News

Naibu Waziri Mhende: Wakulima Wa MuhogoTumieni Mbegu Bora Kukidhi Mahitaji Ya Soko


Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Edwin Mhende akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakulima na wadau wa Muhogo kujadili namna ya kuboresha zao hilo nchini uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Bw.Edwin Rutageruka, akifafanua jambo katika mkutano uliowakutanisha wadau na wakulima wa zao la muhogo nchini kutoka kulia kwake Naibu Katibu mkuu wizara ya viwanda biashara na Uwekezaji uwekezaji Mhe Edwin Mhende Mhe Mwamtum Mahiza mdau wa zao hilo na Balozi Ally Mchumo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Makamu Rais Wa TCCIA Bw. Joseph Kahungwa akiwasilisha mada katika katika mkutano uliowakutanisha wadau wa kilimo cha MUHONGO nchini katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam
Wito umetolewa kwa wakulima wa Zao la Muhogo nchini kulima kwa kuzingatia matumizi ya mbegu zenye uwezo wa kupambana na magonjwa hili kuwapatia mavuno bora.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Edwin Mhede alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa zao la Muhogo ulioratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

“Tulime mbegu inayoendana na mahitaji ya soko, lakini pia yenye uwezo wa kupambana na magojwa,  pia tutie mkazo katika kuongeza thamani ya muhogo katika kuuza nje,” alisema Mhede.

Alisema zao la muhogo kwa sasa siyo la chakula tu bali ni zao la biashara ambapo alieleza kuwa kwa mwaka 2015-2016 zao hilo lilichangia asilimia 14 ya pato la taifa.

Aidha alisema moja ya changamoto kubwa inayokabili kilimo hicho ni magonjwa na namna ya kuhifadhi hivyo alitoa waito kwa watafiti na wadau kujadili namna ya kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

Naibu Katibu Mkuu huyo pia alitoa agizo kwa wadau hao kuunda chama ambacho kitawaunganisha na kuwa na sauti moja kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hicho.

Mhede aliwaahidi kuwa serikali itaendelea kuwaunganisha na wadau mbali mbali ndani na nje ili kuwasaidia katika kutafuta masoko huku akihimiza wawekezaji kujitokeza kwa ajili ya kujenga viwanda vya uchakataji wa muhogo kwa ajili ya kuliongezea thamani zao hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Edwin Rutageruka, alisema kuwa lengo la mkutano huo ilikuwa ni kwa ajili ya kujadili changamoto zinazolikabili zao la Muhogo ili kujua jinsi ya kuzikabili.

Alitaja changamoto hizo kuwa ni changamoto katika uzalishaji wa muhogo, kuongeza thamani ya muhogo, changamoto ya masoko na changamoto ya kupata fedha ya mtaji.

Aidha aliahidi kuwa watayatekeleza maagizo yote ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na yale ambayo watalitarajia kujadili na kukubaliana.

Mkutano huo uliwakutanisha wakulima wa muhogo, wachakataji, wanunuzi, Taasisi za fedha na Taasisi za serikali.

No comments