Breaking News

MUSIBA Ajitosa Kulipa Deni La Mil 15 Kwa Goli kipa Wa Yanga BENNO

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CZI bw Cyprian Musiba amejitolea kusaidia kulipa mshahara wa mlinda mlango wa klabu ya Yanga Afrika Benno kakolanya Kwa kumkabidhi fedha taslimu milioni 2 kati ya milioni 15 alizokuwa akijidai klabu hiyo na kuahidi kumalizia kiasi cha Milioni 13 ndani ya kipindi kifupi kijacho. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam bw Musiba alisema amechukua uhamuzi huo kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa klabu hiyo  hususani katika kipindi hichi cha mpito wakati wanangoja kufanyika kwa uchaguzi na kupata viongozi.

"Nikiwa kama shabiki wa klabu ya Yanga Afrika na mpenda soka nimeona nitoe mchango wangu kusaidia kulipa mshahara wa mchezaji huyu hili aweze kurejea uwanjani kuendelea na majukumu yake ya kuitumikia klabu."Alsema bw Musiba.

Alisema ametoa msaada huo kwa klabu hiyo ana maana kuwa ana mpango wa kugombea wala kutaka kuwania nafasi ya uongozi katika club hiyo bali ametoka kama mpenzi wa klabu hiyo na kwakutambua changamoto iliyopo mbele ya mchezaji huyo ya kumuuguza mama yake.

"Napenda kuwafahamisha wapenzi na wadau wa klabu ya Yanga Afrika kuwa msaada huu nimetoa si kwamba natafuta nafasi ya uongozi au uongozi uliopo autekelezi majukumu yake, bali nimetoa kama mchango wangu kwa klabu si vinginevyo"

Aidha bw Musiba ameomba  uongozi wa klabu hiyo hususani kocha na benchi la ufundi kumpokea mchezaji huyo na kujiunga na wenzake hili aanze kutumikia klabu hiyo kwani swala lake la malipo ameshalipatia ufumbuzi. 

Kwa upande wake mlinda mlango huyo benno kakolanya amemshukuru mkurugenzi huyo kwa kujitolea kulimpa kwani yeye binafsi yupo katika wakati mgumu sana kutokana na mpira kuwa ndio kazi yake na anategemewa na familia.

"Nichukue nafasi hii nikushukuru binafsi mkurugenzi wa CSI bw. Musiba kwa kuamua kuchukua jukumu hili la kunilipa na naomba wapenzi na washabiki wa klabu kuunga mkono klabu ili iweze kuendelea kuwa na matokeo mazuri" Alisema Benno. 

No comments