Serikali Yatoa Sababu Ya Kuzuia Maandamano

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa wanazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane na kuharibu taswira ya nchi.
Akizungumza jana katika harambee
iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya
Pare, wilayani Same, alisema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya
vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba
nchi inaua watu.
‘’Wapo wanaotamani tuvurugane na
tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati
wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu
watuvuruge.
“Tunaangalia sura ambayo adui anaweza
kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo
hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa
ni vitu vyepesi vyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya
yanapojitokeza.”’alisema Dk Mwigulu.
No comments