Rais Magufuli: Msikubali Kuwa Vilaza, Atakayewakwamisha Nambieni Nimshughulikie

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na
kuwaambia viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kuwa wasikubali kuwa vilaza baada ya kugundua Mamlaka ya Chakula na
Dawa, TFDA imekuwa kikwazo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Rais Magufuli
amesema hayo leo Machi 26, 2018 wakati akizundua magari 181 ya Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) ambayo yanategemewa kuanza kusafirisha dawa mijini na vijinini
Akiwa kwenye
uzinduzi huo Rais Magufuli alipokea malalamiko kuwa zipo baadhi ya taasisi za
serikali zimekuwa zikichangia kukwamisha ucheleweshwaji wa dawa ambazo
zinaletwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
"Nimesikia
saa zingine kunakuwa na ucheleweshwaji kati ya taasisi fulani fulani ndani ya
serikali taasisi ya vyakula TFDA, mnaleta madawa halafu mnashindwa kupata
kibali bandarini, madawa yanacheleweshwa inawezekana 'expire date' yake inafika
madawa bado yamezuiliwa pale bandarini.
" Mimi atakae
zuia madawa haya niambieni ili nijue chombo gani cha serikali, niambieni tu
huyo aliyezuia nione ili na mimi nimzuie yeye moja kwa moja,kuna mambo mengine
ni rahisi sana wala msilalamike bali mwambie Waziri au Katibu Mkuu"
alisema Rais Magufuli
Magufuli
aliendelea kuweka wazi kuwa watu ambao wanakwamisha na kuchelewesha dawa kutoka
ni watu ambao pia wanatoka katika wizara hiyo hiyo wa Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
"Hata
aliyempa nguvu ya kuzuia dawa wapo chini ya wizara yenu yaani ni nyinyi
wenyewe, basi nyinyi vilaza sasa mtu yupo chini yenu, yaani mtu anayezuia yupo
kwako anayezuiliwa yupo kwako bado mnakaa mnaimba nini.
"Mimi nataka
haya niyashughulikie unajua mambo mengine mnakwamishana nyinyi wenyewe kama ni
TRA mwambie Katibu Mkuu, mwambie Waziri wa Afya, mwambie Waziri wa Fedha tufike
mahali tusikwamishane, kwa sababu anaweza akawa amekwamisha madawa yenu lakini
madawa ya mtu binafsi anayaruhusu siku hiyo hiyo sasa hili ni lenu wala
halihitaji kufika kwangu" alisisitiza Magufuli
No comments