Mhe Said Soud Said Mwenyekiti Taifa Chama Cha AFP
Mwenyekiti Wa
Chama Cha Wakulima Taifa (AFP) Mhe. Said akimzungumza na wajumbe wa Mkutano
Mkuu Taifa mara baada ya kutangazwa mshindi wa kishido kwa kupata kura 97 kati
ya 102 jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Wajumbe Wa Mkutano
Mkuu Taifa Wa Chama Cha Wakulima Tanzania (AFP) Wamemchagua Mhe. Said Soud Said
Kuongoza Tena Chama Hicho Kwa Kipindi Cha Miaka Nne Baada Ya Kupata Kura 97
Kati Ya Kura 102 Za Wajumbe Wote Wa Mkutano Mkuu Wa Taifa.
Mhe Said Ambaye
Alikuwa Anatetea Nafasi Hiyo Katika Uchaguzi Huo Alikuwa Mgombea Pekee Wa Nafasi
Ya Mwenyekiti Taifa Alipata Kura Za Ndio 97, Kura 3 Za Hapana, Wajumbe 2
Hawakupiga Kura.
Pia Wajumbe Wa
Mkutano Huo Wamemchagua Bw. Kilindo Saidi Kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara,
Na Mhe. Juma Saidi Amary Kuwa Makamu Mwenyekiti Uoande Wa Zanzibar.
Akizungumza Mara
Baada Ya Kutangazwa Mshindi Mwenyekiti Wa Chama Cha Wakulima Taifa (AFP) Mhe.Said
Soud Said Aliwashukuru Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Taifa Kwa Kuwa Na Imani Nae
Na Kumpa Kura Za Ndio Za Kutosha.
Alisema Ataendelea
Kudumisha Umoja Na Mshikamano Uliopo Ndani Ya Chama Hicho Hili Kuweza Kufikia
Malengo Ya Kikatiba Ya Kuanzishwa Kwa Chama Hicho Hili Kiweze Kushika Dola.
Alisema Umoja Na
Mshikamano Ndio Silaha Pekee Kwao Kuweza Kufikia Malengo Waliojiwekea Kama
Chama Sambamba Na Kutekeleza Sera Za Chama Hicho Ambacho Kwa Asilimia Kubwa
Wanachama Wake Ni Wakulima.
Mkutano Huo
Umewapitisha Mhe. Rashid Rai Kuendelealea Kuwa Katibu Mkuu Taifa Kwa Kipindi
Kingine Cha Maiaka Nne, Sambamba Na Abdul Ngakolwa Naibu Katibu Mkuu Bara Na
Mhe Salum Masuud Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Pia Wajumbe Wa
Mkutano Huo Pia Wamewachagua Bw. Isidory Mhemela Kuwa Mwenyekiti Wa Vijana Taifa
Sambamba Na Bi Rehema Nassoro Ligawandu Kuwa Katibu Wa Vijana Taifa.
Jumla Ya Wajumbe
102 Kutoka Tanzania Bara Na Zanzibar Wameudhulia Mkutano Huo Ambao Umefanyika
Jijini Dar Es Salaam
Wajumbe
Wa Mkutano Mkuu Wa Chama Cha Wakulima Tananzania (AFP) Wakifatilia Mada
Mbalimbali Katika Mkutano Huo Uliofanyika 10 Feb 2018 Jijini Dar Es Salaam
Mwenyekiti Wa Mkoa
Wa Lindi Mhe. Abdull Azizi, Kushoto Akiwa Na Msajili Msaidizi wa Vyama Vya
Siasa Bw. Siyst Leonard Nyahoza Nje Ya Ukumbi Ulikofanyika Mkutano Mkuu Wa Taifa Chama Cha Wakuliama Tanzania (AFP)
Jijini Dar es salaam.
No comments